NAMNA YA KUOMBA


          1. NENO LA MSINGI

YOHANA 16:24

“Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu: OMBENI, NANYI MTAPATA; furaha yenu iwe timilifu”.

Maneno haya aliyasema Yesu Kristo mwenyewe akiwaambia Wanafunzi wake. Tunaona katika maneno haya kwamba, kila mwanafunzi wa Yesu au mtu aliyeokoka, ana haki ya kumwomba Baba yetu aliye mbinguni kwa Jina la Yesu Kristo na akapokea jibu. Yesu hasemi kwamba mtu fulani tu aliyeokoka akiomba, ndiye atakayepata jibu, bali YEYOTE.

MARKO 11:23

“Amin, nawaambia, YEYOTE atakayeuambia mlima huu, ng’oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake. Kwa sababu hiyo nawaambia, yoyote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.”

Maandiko mengi yanadhihirisha jinsi ambavyo kila mtu aliyeokoka alivyo na haki ya kuomba na kupokea jibu na wala siyo mtu fulani pekee. [Angalia mifano katika YOHANA 14:12-14; MATHAYO 7:8-11].

ANGALIA TENA LUKA 11:10; “ Kwa kuwa KILA AOMBAYE HUPOKEA…….”.

Unaona! Kila mtoto wa Mungu, yaani kila mtu aliyeokoka, akiomba, hupokea. Huu ni UHONDO maalum kwa watoto wa Mungu tu. Mtu ambaye hajaokoka, ametenganishwa kabisa na Mungu kutokana na maovu yake. Kutokana na dhambi za mtu ambaye hajaokoka kumfarikisha au kumtenganisha na Mungu, sala zake ni machukizo mbele za Mungu na hazisikilizwi kabisa. [SOMA ISAYA 59:2; MITHALI 28:9; MITHALI 15:29; YOHANA 9:31]. Sala pekee ambayo inasikilizwa na Mungu inapotoka kwa mtu ambaye hajaokoka, ni pale anapotubu dhambi zake na kuwa tayari kuziacha na kuomba damu ya Yesu imsafishe uovu wake; ili aokolewe kutoka katika mauti ya milele [1 YOHANA 1:7-9]. Mtu ambaye hajaokoka, akimpokea Yesu Kristo kuwa Bwana au Mtawala wake na mwokozi wake ndipo anapofanyika MTOTO WA MUNGU na kuanza kufaidi uhondo wa kujibiwa maombi na Baba yetu aliye mbinguni [YOHANA 1:12]. Kabla ya kuokoka, mtu anakuwa ni mtoto wa Ibilisi, na siyo mtoto wa Mungu [YOHANA 8:44]. Kwa sababu hiyo ili uingie katika mpango wa Mungu wa kukupa majibu ya maombi, kwanza ni lazima ukubali kuokolewa na kuwa mtoto wake.

KUTEGEMEA KUOMBEWA NA MWINGINE WAKATI WOTE

Ni huzuni kwamba, wako watoto wa Mungu ambao wanafikiria kwamba wao hawawezi kusikilizwa na Mungu na kujibiwa; mpaka waombewe na mtoto wa Mungu mwingine. Huku ni kukosa ufahamu. Hakuna upendeleo kwa Mungu. Mtoto yeyote katika familia ya Mungu anakubaliwa na Baba aliye Mbinguni. Hakuna mtoto anayekubaliwa na Mungu zaidi anapoomba kuliko mwingine [SOMA MATENDO 10:34-35; WARUMI 2:10-11; KUMB.10:17]. Biblia inasema Mungu hapokei uso wa mwanadamu, yaani hamuoni mtoto wake mmoja kuwa ni bora kuliko wengine kiasi ya kwamba wengine asiwajali [WAGALATIA 2:6]. Eliya alipoomba mvua isinye kwa miaka 31/2; halafu akaomba tena mbingu zikatoa mvua; alikuwa katika hali ya mtoto wa Mungu kama yeyote yule. Alikuwa mwenye tabia moja na sisi, na Mungu hakufanya hayo kwa sababu aliomba Eliya! [YAKOBO 5:17-18].

Watu wengi waliookoka, wanatembea huko na huko katika mikutano wakihitaji kuombewa na watu wengine. Miongoni mwao, wako wanaofikiri sala ya mzungu fulani kutoka Marekani au Uingereza ndiyo ataisikia Mungu zaidi kuliko sala yake. Huku ni kukosa ufahamu. Mungu hapokei uso wa mwanadamu wala hana upendeleo. Kila aaminiye, akiomba hupokea. Ukifanya utafiti, utagundua kwamba, mara nyingi watu ambao wanapokea miujiza wanapoombewa na wengine; ni wale ambao hawajaokoka kabisa, au wale waliookoka lakini wakiwa na muda mfupi sana katika wokovu. Sababu ni kwamba, baada ya mtu kuwa na muda mrefu katika wokovu; unatazamiwa na Mungu kuchukua mwenyewe chakula na kukila bila kungoja kulishwa. Biblia inasema uponyaji ni chakula cha watoto wa Mungu [MATHAYO15:26]. Katika hali ya asili, mtoto anapozaliwa, katika uchanga hulishwa kwa kijiko na mtu mwingine, kwa sababu hawezi kujilisha mwenyewe. Mtoto huyo anapokua, anatazamiwa achukue kijiko na kula mwenyewe. Haitapendeza kumwona mtoto mwenye miaka kumi, akilishwa chakula na mtu mwingine. Vivyo hivyo katika maombi, kila mtu aliyeokoka anatazamiwa kuomba mwenyewe na kuchukua jibu lake. Kwa kukosa maarifa, watu wengi wa Mungu wameangamia [HOSEA 4:6]; na kukosa majibu ya maombi yao. Yafuatayo ni maarifa unayopaswa kuwa nayo ili upate majibu ya maombi yako kila mara.

A: MAMBO MANNE YA KUYAFAHAMU KABLA YA KUMWOMBA MUNGU LOLOTE
1. Mfahamu Vizuri Mungu Baba na Mungu Mwana

Kwa kuwa tunamwomba Mungu Baba kwa jina la Mungu Mwana-Yesu Kristo, ni vema sana kuwafahamu vizuri ili tuwe na hakika ya kujibiwa. Ufahamu ulio nao kuhusu mtu unayekwenda kumwomba hitaji lako, unaweza ukakupa imani ya kupokea kwake au ukakupunguzia imani hata ya kwenda kumweleza hitaji lako. Ukifahamu kwamba mtu fulani ni katili, ufahamu huo unatosha kuondoa ujasiri wa kumwomba lolote. Kwa kukosa kuwafahamu vizuri Mungu Baba na Mungu Mwana, watu wengi waliookoka wamekosa msingi mzuri wa kujibiwa maombi yao. Kinyume na inavyopasa, msingi wao wa kuomba unakuwa ni manung’uniko ambayo huleta maangamizo badala ya mafanikio [SOMA 1 WAKORINTHO 10:10]. Ukiwafahamu vizuri Mungu Baba na Mungu Mwana, ufahamu huo pekee, utakufanya uwe na hakika ya mambo unayotarajia kuyapata; ingawa hayajaonekana bado. Hii ndiyo inayoitwa IMANI ambayo ni msingi muhimu wa kupewa majibu yetu [WAEBRANIA 11:1,6]. Imani ni kuamini jinsi Neno la Mungu linavyoeleza kuhusu Mungu alivyo kwetu. Ukiwafahamu Mungu Baba na Mwana walivyo huwezi kunung’unika, kubabaika na kukata tamaa. Kunung’unika, Kubabaika na Kukata tamaa; ni kinyume kabisa na Imani. Watu wanaonung’unika, kubabaika na kukata tamaa, ni watu wasiomfahamu Mungu alivyo. Usiwe miongoni mwa watu wa jinsi hiyo, ambao hawawezi kupata majibu ya maombi yao.



Inakubidi basi, kuyafahamu yafuatayo na kuyaamini kabla ya kuomba; ili upate Majibu yaMaombi yako:

Mungu Baba hujishughulisha SANA na kila jambo tunalolihitaji, liwe dogo au kubwa. Wakati wote, fahamu kwamba hitaji ulilonalo anapenda kulishughulikia mno. Anataka tu, umtwike YEYE fadhaiko ulilo nalo. [SOMA 1 PETRO 5:6-7].

(b) Ni mapenzi ya Mungu Baba, kukupa haja za moyo wako na kukuona una furaha baada ya kujibiwa maombi [SOMA ZABURI 37:4; YOHANA 16:24].

(c) Mungu Baba anawahurumia watu waliookolewa kama vile Baba awahurumiavyo watoto wake [SOMA ZABURI 103:13]. Linalofurahisha zaidi ni kwamba, Mungu Baba; ni Baba mwenye uwezo wote, tofauti na baba wa duniani ambao wanaweza kuwa na huruma kwa watoto wao, lakini wakakosa uwezo wa kuwasaidia; wakabaki kusema “POLE”, bali huruma ya Mungu huambatana na UWEZO wa kutupa mahitaji yetu; hata yakiwa mazito kiasi gani. [ANGALIA MFANO LUKA 7:13-15].

(d) Mungu kamwe hawasahau, hawaachi, hawapungukii wala hawatupi watoto wake yaani watu waliookoka. Unapokuja mbele za Mungu ukiwa unajiona umeachwa, umesahauliwa au umetupwa; basi ujue unampa nafasi shetani ya kukuangamiza kwa kukosa maarifa ya Neno la Mungu. Tunaweza tu kumshinda shetani kwa “Imeandikwa” yaani kwa Neno la Mungu, kama Yesu alivyomshinda alivyokuwa anajaribiwa na Ibilisi nyikani. Mbinu kubwa ya Ibilisi anayotumia kumshinda mtu aliyeokoka, ni kumfanya akiri tofauti na “Imeandikwa”. Unachotakiwa kufahamu kuanzia leo ni kwamba, Imeandikwa kuwa Mungu hawezi kumsahau, kumuacha au kumtupa mtoto wake, yaani mtu aliyeokoka. Wewe unaweza kumwacha, lakini yeye hawezi kukuacha katika mahitaji unapokaa ndani yake. [SOMA KWA MAKINI ZABURI 94:14; KUMBUKUMBU 31:8; ISAYA 49:14-16; ZABURI 37:25; 1 SAMWELI 12:21-22; 1 WAFALME 6:13; ZABURI 37:28].

(e) Ikiwa Mungu Baba alimtoa mwanawe wa pekee Yesu Kristo ili afe kwa ajili ya dhambi zetu, je hatazidi sana kutupa mambo mengine tunayoyahitaji, ambayo thamani yake siyo kubwa kama thamani ya mwanae wa pekee? [SOMA WARUMI 8:32].

(f) Yesu Kristo ni mzaliwa wa kwanza katika uzao wa Adamu wa pili yaani uzao wa watu waliookoka. Ni kusema kwamba, Yeye ni NDUGU yetu. Yeye ni KAKA YETU wa kwanza kuzaliwa. [SOMA WARUMI 8:29; WAEBRANIA 2:11]. Tafakari jinsi alivyo ndugu wa kwanza kuzaliwa katika familia, hasa anapokuwa wa kiume. Mahitaji yote ya wadogo zake, huyabeba yeye. Ni kaka yupi mwenye uwezo wote wa kuwasaidia wadogo zake, ambaye atawaacha ndugu zake bila msaada? Ikiwa kaka wa duniani wasiokuwa na uwezo wote, wanajitahidi kuwasaidia wadogo zao; ni zaidi sana kwa kaka yetu Yesu Kristo mwenye upendo wote na uwezo wote mbinguni na duniani. Anahusika MNO NA KILA HITAJI walilo nalo wadogo zake. Ndiyo maana anamwita mdogo wake yeyote mwenye kusumbuka na kulemewa na mzigo wowote, aende kwake ampumzishe. [MATHAYO 11:28]. Yesu anataka tumtwike mizigo yetu yote na masumbufu yetu yote, kama jinsi ambavyo Baba anavyotaka tumtwike fadhaa zetu zote!

2. Fahamu jinsi ulivyo wa thamani mbele za Mungu

(a) Wewe ni TAJI YA UZURI katika mkono wa BWANA [ISAYA 62:3]. Jiulize mwenyewe, taji ya uzuri utakubali ichafuliwe na tope au ichanwe? Utaitunza na kuiangalia namna gani?

Wewe ni KILEMBA CHA KIFALME mkononi mwa Mungu wako [ISAYA 62:3]. Kilemba cha kifalme ni kitu cha thamani mno. Kinazidi thamani yake kinapokuwa ni kilemba cha kifalme cha Mungu. Wewe ni kilemba cha Kifalme cha Mungu. Wewe ni wa thamani mno machoni pa Mungu. Jiulize mwenyewe, Mungu ataacha kukitunza kilemba chake cha kifalme?

(b) Anayekugusa wewe na kukutesa, kukuonea, au kukukosesha furaha, anakuwa anaigusa mboni ya jicho la Mungu [ZEKARIA 2:8]. Ikiwa wewe huwezi kukubali kuweka kidole kwenye mboni ya jicho la Mungu. Atafukuzwa kwa utisho mkuu.

(c) Katika mpango wa Mungu, Yesu alikuokoa wewe na kukutoa mahali palipokuwa pakame na jangwa tupu lisilokuwa na matumaini; na kukulaza kwenye majani mabichi. Hataki tena upungukiwe na kitu [ZABURI 23:1-2]. Zaidi ya hayo, kwa kuwa wewe ni wa thamani mno kwake, anakuzunguka na kukulinda kwa uwezo wake wote. Mpango wake, ni kukutunza na kukuhifadhi kama mboni ya jicho [SOMA KUMBUKUMBU 32:10]. Jiulize mwenyewe, Je, unaitunza namna gani mboni ya jicho lako? Kipande kidogo tu cha mchanga kikiingia jichoni, utahangaika mno mpaka kitolewe. Utairuhusu miiba ikaribie kwenye mboni ya jicho lako? Mboni ya jicho ikiingiwa na vumbi kidogo tu, jicho lote hujaa machozi na mwili wote kuhuzunika. Furaha huja tu pale vumbi linapotoka. Ndivyo alivyo Yesu pia unaposumbuliwa wewe mboni ya jicho lake, yeye pia hulia machozi pamoja nawe na kuhakikisha kila kinachokusumbua kinatoweka [YOHANA 11:33-36, 43-44].

(e) Wewe ni KITO AU JIWE LA THAMANI LINALOMETAMETA katika nchi ya Mungu[ZEKARIA 9:16]. Jiwe la thamani linaangaliwaje? Hazina inashughulikiwaje?

(f) Wewe ni HAZINA YA MUNGU [SOMA MALAKI 3:16]. Hazina inalindwaje? Hazina inaangaliwaje? Hazina inatunzwaje? Hazina inashughulikiwaje?

(g) Wewe ni MALI ILIYONUNULIWA KWA THAMANI KUBWA. Ulinunuliwa kwa damu ya YESU ya thamani. [SOMA 1 WAKORINTHO 7:23; 1 WAKORINTHO 6:20]. Jiulize mwenyewe! Mali uliyoinunua kwa thamani kubwa, unailinda na kuitunza namna gani? Mwanadamu anaweza kuwa mzembe, asijue sana kutunza mali; lakini Mungu asiye mzembe kamwe, hakika atakutunza. Wewe ni wa thamani mno kwake!

Wewe ni BIBI-HARUSI, MKE WA MWANA-KONDOO yaani MKE WA YESU [SOMA UFUNUO 21:9]. Biblia inasema, “Kama Bwana-Arusi amfurahiavyo Bibi-Arusi, ndivyo Mungu anavyokufurahia wewe.” [SOMA ISAYA 62:5]. Ikiwa Yesu anakufurahia hivi kama Bibi-Arusi wake, je atakuacha kabisa na asikujali au asikupe mahitaji yake? Dalili ya kumfurahia Bibi-Arusi, ni kuhusika sana na mahitaji yake. Bibi-Arusi anapoomba lolote kwa Bwana-Arusi, mara moja Bwana-Arusi hufanya jitihada yote ili ampe na kumfurahisha. Mabwana-Arusi wa duniani hawana uwezo wote, hivyo hukwama katika kuwatekelezea mahitaji yao yote Mabibi-Arusi wao; lakini Bwana-Arusi Yesu Kristo mwenye uwezo wote, kamwe hashindwi. Lolote unalolihitaji kwake, atakupa ili akufurahishe. Mungu ni MUME WAKO! [SOMA YEREMIA 3:14]. Huu ni ukweli wa ajabu! Ikiwa mumeo ni Rais wa Nchi, utakuwa na hakika ya kutunzwa, kuangaliwa na kupewa mahitaji yako! Hata hivyo Rais wa Nchi ana mpaka. Hawezi kukupa mahitaji yako yote. Sasa tafakari ukweli huu kwamba Mungu aliye muumba wa mbingu na nchi ni mumeo! Una haki ya kuringa, kuwa na mume wa namna hii mwenye uwezo wote. Je atashindwa kukupa nini? Ana uwezo wa kutuma watumishi wake malaika, wakuletee chochote ukitakacho.

3. Fahamu kwamba hakuna gumu lisilowezekana kwa Mungu:

Usiupime kamwe uwezo wa Mungu kwa kuulinganisha na uwezo wa mwanadamu. Kufanya hivyo, ni kama kuulinganisha uwezo wa kuangaza kwa JUA na KOROBOI! Kulinganisha kiasi cha uwezo wa Mungu wa kufanya jambo na uwezo wa mwanadamu, ni kama kulinganisha kiasi cha maji kinachotosha kuijaza bahari, na kile kinachotosha kujaza kikombe. Kwake Mungu, hakuna neno ‘HAIWEZEKANI’. Hili ni neno la kibinadamu tu! Mungu anasema ingawa jambo linaweza kuwa haliwezekani mbele za wanadamu na kuwa gumu mno lakini siyo mbele za Mungu. Angalia maandiko.

ZEKARIA 8:6

“Bwana wa majeshi asema hivi, Ingawa hili ni neno lililo gumu mbele ya macho ya mabaki ya watu hawa siku hizo, je! liwe neno gumu mbele ya macho yangu? asema BWANA wa majeshi.

“SOMA PIA YEREMIA 32:17, 27; AYUBU 42:2; MATHAYO 19:26; LUKA 1:37”.

4. Fahamu kwamba magonjwa na umasikini siyo mapenzi ya Mungu kwako:

Magonjwa na umasikini au kutofanikiwa, ni sehemu ya LAANA juu ya mtu asiyetaka kuisikiliza sauti ya BWANA Mungu na kufanya maagizo yake [KUMBUKUMBU 28:15-28]. Yesu alifanyika laana kwa ajili yetu kwa kupigiliwa msalabani ili baraka zitufikie [WAGALATIA 3:13-14]. Kwa kupigwa kwake Yesu na hatimaye kusulubishwa msalabani, alitukomboa kutoka katika:-

(a) Dhambi [MATHAYO 26:28; 1 PETRO 2:24].

(b) Magonjwa na udhaifu wote [MATHAYO 8:14-17; ISAYA 53:4-5;

1 PETRO 2:24].

(c) Umasikini [ 2 WAKORINTHO 8:9].

Magonjwa na udhaifu wote, umasikini na dhambi; zote ni kazi za Ibilisi ambazo zilivunjwa na Mwana wa Mungu [1YOHANA 3:8]. Watu tuliookolewa, hatuko tena chini ya laana. Hivyo kama unavyozikataa na kuzipinga dhambi,vivyo hivyo inakupasa kuyakataa na KUYAPINGA MAGONJWA na Udhaifu wote, na kuukataa umasikini. Hivyo usiseme “Labda ni mapenzi ya Mungu niugue” au “Huenda anataka kunifundisha kwa ugonjwa”. Ni mapenzi ya Mungu UWE MZIMA WA AFYA – Yeye anaitwa YEHOVA-RAPHA AU “BWANA NIKUPONYAYE” [SOMA KUTOKA 15:26; YEREMIA 30:17; YEREMIA 33:6; ZABURI 103:3; YOHANA 10:10; 3 YOHANA 1:2].

Mungu ana njia nyingi za kukufundisha. Hakufundishi kwa kumruhusu shetani akuletee magonjwa! Ukisema ni mapenzi ya Mungu uugue, basi ujue unazidi kumpa nafasi shetani akutese zaidi. Mapenzi ya Mungu, ni Neno la Mungu. Shetani akijua kwamba hulijui neno lililoandikwa, atakutesa! Usimpe nafasi Ibilisi kwa kuzungumza yaliyo kinyume na Neno la Mungu. Mara zote, yapinge magonjwa ukijua kwa kufanya hivyo unampinga shetani; naye atakimbia. Shetani ndiye mleta magonjwa yote. Shetani ndiye aliyeleta magonjwa juu ya Ayubu na kutofanikiwa kote. Ayubu hakujua akasema ni Mungu! Usiwe kama Ayubu. Mjue mbaya wako Shetani! [Angalia WAEFESO 4:27; YAKOBO 4:7; AYUBU 1:12-16; AYUBU 2:2,7]. Hivyo kumbuka kwamba usitumie “Ikiwa ni mapenzi yako” katika kuomba juu ya ugonjwa. Tunatumia maneno haya pale tu tusipokuwa na uhakika wa jambo. Uhakika juu ya ugonjwa uko tayari katika Neno. Ni mapenzi ya Mungu uwe mzima.

B. UKIYAJUA HAYA MWELEZE MUNGU HAJA ZAKO KWA MAOMBI:

Bila mashaka ya kupokea majibu, wewe kama Bibi Arusi mwendee Mume wako Mungu, na kumwelezea unalolihitaji. Maombi ni mazungumzo na Mungu. Zungumza naye kama jinsi ambavyo unavyoweza kuzungumza na mumeo, Rafiki yako, Baba yako au Kaka yako. Usimwendee huku ukinung’unika, ukilia na kubabaika; kiasi ya kwamba hata unalolihitaji halifahamiki! Usiseme yeye anajua yote, hivyo huna haja ya kumweleza kitu. Hivyo siyo sawa na Neno la Mungu. Utampa nafasi Shetani kukupiga kwa kusema hivyo, maana hulijui Neno la Mungu. Mpango wa Mungu wa sisi kupokea, ni KUMWOMBA tukimweleza mambo yote tunayoyahitaji [ISAYA 43:26; YOHANA 16:23-24; YOHANA 15:7]. Kumbuka Neno linavyosema “Kila aombaye hupokea.” Ni kwa sababu hii huna haja ya kutaka watakatifu fulani waliokufa wakuombee! Siyo Bikira Maria, Petro, Paulo au yeyote. Yesu mwenyewe kwa pendo lake, ndiye pia Mwombezi wetu kwa Baba. Hakuna mwingine mbinguni! [1 YOHANA 2:1]. Kwa Imani tu, zungumza na Mungu bila kutumia vitu vingine na kuviweka kati yako na Mungu kwa mfano Rozari, Maji ya Baraka n.k. Aliye kati yetu na Mungu anapaswa kuwa YESU tu! Watu wengine husema kwamba hawajui kuomba kwa kutokujua maana ya maombi. Kama ulivyotangulia kufahamu, maombi ni mazungumzo. Mke anazungumzaje na Mumewe? Ebu angalia mfano huu:- “Mume wangu, naomba fedha nikanunue mafuta ya kujipaka. Ngozi imechubuka sana kutokana na jua kali. Nimeona mafuta mazuri yanauzwa kwa shilingi mia moja.”

Kwa jinsi hii hii, ndivyo tunavyozungumza na Mungu. Ni jinsi ile ile mtoto anavyomwomba Baba yake kalamu ya kuandikia shuleni.

C. TUMIA MAMLAKA ULIYO NAYO JUU YA SHETANI KATIKA MAGONJWA NA ONDOA VIZUIZI VYAKE VYOTE VYA MAJIBU.

Hapo mwanzo, Adamu alikuwa na mfano wa Mungu katika utakatifu mpaka pale alipotenda dhambi kwa kutumia vibaya hiari yake ya kuchagua jambo la kufanya. Akachagua kuliasi Neno la Mungu, tendo ambalo ndilo linaloitwa dhambi. Kabla Adamu hajafanya dhambi, alikuwa ni MTAWALA. Chochote katika nchi kilipaswa kumtii Adamu. Hii ni pamoja na Shetani. Adamu alipofanya dhambi na kukubali Neno la Shetani, alipoteza mamlaka ya utawala aliyokuwa nayo na akayachukua Shetani. [MWANZO 1:26-27]. Alipokuja Yesu na kututoa katika utumwa wa dhambi, na kuzivunja kazi za Ibilisi aliyetutumikisha wote tuliozaliwa kutokana na Adamu; alifanya jambo jingine zuri. Aliturudishia mamlaka aliyotunyang’anya Shetani. Ndiyo maana Yesu alisema “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani baada ya kufufuka [MATHAYO 28:18]. Sasa mamlaka hii aliyoichukua Yesu ni ile aliyokuwa ametunyang’anya Shetani. Kwa kumshinda Shetani na kazi zake zote, Yesu alimnyang’anya mamlaka Shetani na kutupa mamlaka hiyo ambayo pia inaitwa “AMRI”. Kwa mamlaka hii au “AMRI” aliyoturudishia kila mtu aliyeokoka ana uwezo wa kumkanyanga nyoka yuleyule aliyetukanyaga mwanzo. Nguvu zote za Shetani, hazina uwezo juu ya mtu aliyeokoka.

LUKA 10:18-19

“Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme. Tazama nimewapa AMRI ya kukanyanga nyoka na nge, na NGUVU ZOTE ZA YULE ADUI (SHETANI), wala hakuna kitu kitakachowadhuru.” Nguvu zozote za Shetani hata kama zingekuja kwa vitisho kama umeme, ziko chini ya “AMRI” au “MAMLAKA” ya mtu aliyeokoka. Unapolitumia Jina la Yesu kwa Mamlaka au Amri juu ya pepo wanaosababisha tatizo ulilo nalo, pepo hao watakutii na kuondoka [SOMA LUKA 10:17]. Magonjwa mengi husababishwa na pepo wa udhaifu [SOMA LUKA 13:11; MATHAYO 12:22;MARKO 9:17, 25; LUKA 11:14]. Unapokuwa umeelemewa na ugonjwa wowote iwe ni homa au ugonjwa wowote, au unapokuwa unaomba kwa ajili ya ugonjwa alio nao mwenzio; haitoshi tu kumwomba Mungu auponye ugonjwa huo, ila inakubidi pia UTUMIE MAMLAKA ULIYO NAYO JUU YA SHETANI NA KUUKEMEA UGONJWA HUO NA KUUAMURU KWA AMRI KWAMBA UHAME. [Angalia mfano katika [LUKA 4:38-39].

MFANO WA MAMLAKA KATIKA ULIMWENGU HUU:

Waangalie askari wa Usalama Barabarani au askari wa trafiki. Hata kama umbo la askari ni dogo namna gani, kwa kutumia mamlaka aliyopewa na Serikali, anaponyosha mkono mtupu usio na chochote, gari kubwa lenye tela nyuma na linaloendeshwa na mtu mwenye umbo kubwa husimama pale pale. Vivyo hivyo kwa mtu aliyeokoka. Hata kama ukiwa na umbo dogo namna gani au umeokoka leo tu au jana, unapoamuru pepo wa udhaifu au kazi yoyote ya Shetani ikuachie bila mashaka yoyote, kazi hiyo ya Shetani itahama. Mamlaka uliyopewa na Yesu ni kubwa mno. Unapolitumia Jina la Yesu, ni kwamba unamwakilisha Yesu mwenyewe kama jinsi ambavyo askari wa Usalama Barabarani anavyoiwakilisha Serikali. Askari wa Usalama Barabarani anaponyosha mkono kuamuru gari kusimama, huwa hana mashaka ndani yake kwamba labda gari hilo litaendelea kwenda. Ni lazima dreva huyo atatii na kulisimamisha gari. Vivyo hivyo kwako, inakupasa kutoa mashaka unapomkemea Shetani kuhama; naye lazima atakutii [LUKA 10:17]. Unapokuwa pia ukiomba, kumbuka kukemea namna zozote za vizuizi vya Shetani juu ya majibu ya maombi yako. Shetani hutumia wakuu wake wa giza walio chini yake KUCHELEWESHA MAJIBU ya Maombi ya Watakatifu [ANGALIA MFANO KATIKA DANIEL 10:12-13].

D. BAADA YA MAOMBI, AMINI KWAMBA UMEPOKEA MAJIBU NA USIKUBALI KUTEGWA NA SHETANI KWA MANENO

Biblia inasema katika MARKO 11:24, “Kwa sababu hiyo nawaambia, yoyote myaombayo mkisali, AMININI YA KWAMBA MNAYAPOKEA nayo yatakuwa yenu”. Hali unayokuwa nayo BAADA ya maombi ni muhimu sana kama unataka kuona muujiza wako au jibu la maombi yako. Kamwe usikubali kuongozwa na milango mitano ya fahamu baada ya maombi. Usiongozwe na KUONA AU HISIA! Ya kwamba unajisikiaje au unajionaje baada ya maombi, hayo siyo muhimu. Hatuenendi kwa kuona bali kwa imani [SOMA 2 WAKORINTHO 5:7] Wakati mmoja, Yesu aliulaani mtini usiokuwa na matunda. Wanafunzi wakasikia alivyotoa amri juu ya mti ule, lakini halikuonekana badiliko lolote la kuonekana machoni wakati huo huo. Kesho yake asubuhi wanafunzi wale ndipo wakashangaa kuona mtini ule umenyauka kutoka shinani. Wakamwambia Yesu kwamba mtini ule umenyauka (BAADA YA KUONA!) . Yesu akawajibu “MWAMININI MUNGU”. [SOMA MARKO 11:12-14, 20-21]. Maana yake nini? Palepale Yesu alipotoa amri, mti ule ulinyauka kutoka kwenye MIZIZI! Macho hayaoni mizizi ya mti maana iko chini ya udongo. Kesho yake, kunyauka huko kulikwisha fika kwenye shina na kwenye matawi mahali ambapo macho yanapoona. Jina la Yesu katika amri linashughulikia MZIZI WA TATIZO ili kukuweka huru kabisa. Macho yanachukua muda kuona wakati mwingine. Macho hungoja kuona shina na matawi. Kungoja kuona kwa macho siyo Imani na huua kabisa matokeo ya maombi. Kumbuka baada ya maombi kwamba hata kama majani kwenye matawi yanaendelea kuwa kijani kibichi, yatakauka tu kwa kuwa mizizi ya mti imenyauka. Usikiangalie kichwa au tumbo linaloendelea kuuma baada ya maombi. Mzizi umenyauka! Tumbo lazima litaacha kuuma.

Unalotakiwa kufanya baada ya maombi ni KUKIRI USHINDI kwa maneno ya kinywa chako. Mungu aliumba mbingu na nchi kwa Neno. Na iwe hivi ikawa hivyo. Neno la Mungu lina uwezo wa kuumba. Kwa jinsi hiyo hiyo, mtoto wa Mungu ana uwezo wa kuumba kwa maneno yake. Kwa maneno yako, utashiba mema au mabaya [SOMA KWA MAKINI MITHALI 18:20-21]. Baada ya maombi, Shetani hungoja kukutega kwa maneno ya kinywa chako. Maneno yako yasiyokiri ushindi humfanya mwindaji au mtega mitego Shetani kukushinda tena na kuendelea kukuonea. Kujiponya katika mtego wake, ni kukiri ushindi.

MITHALI 6:2,5:

“Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako. Ujiponye kama paa na mkono wa mwindaji, na kama ndege katika mkono wa mtega mitego”.

Jambo muhimu la kukumbuka ni kwamba kukiri ushindi kwa maneno ya kinywa chako siyo kibali cha kusema uongo. Ikiwa ulikuwa unaomba nyumba na hujaipata baada ya maombi, usiseme “Nimekwisha pata nyumba nzuri sana iko Sinza, Dar es Salaam.” Huo ni uongo ambao unampa nafasi zaidi Shetani ya kukukosesha muujiza. Kama bado kichwa kinauma na homa inaendelea baada ya maombi unapoulizwa usiseme “Kuuma kichwa na homa, vyote vilikwisha toweka zamani”. Kama bado ni kipofu baada ya maombi usiseme “Ninaona sasa bila matatizo.” Huo wote ni uongo. Biblia inatukataza kumtetea Mungu kwa kusema uongo kwa ajili yake. [AYUBU 13:7-8].

Kukiri ushindi kwa maneno yako baada ya maombi, ni kukiri maneno ya Mungu ya ushindi bila kujali mazingira uliyo nayo au hali uliyo nayo baada ya maombi. Kwa mfano, “ Kwa kupigwa kwake,mimi niliponywa”[1 PETRO 2:24]; “Aliyachukua masikitiko yangu na huzuni zangu. Kwa kupigwa kwake mimi nilipona” [ISAYA 53:4-5]; “Siku za njaa nitashiba, sitaaibika wakati wa ubaya.” [ZABURI 36:19]; “Wamtafutao BWANA hawatahitaji KITU CHOCHOTE kilicho chema”. [ZABURI 34:10]; “Yesu amekuja ili niwe na uzima, tena niwe nao tele”. Mungu anapenda nifanikiwe katika mambo yote. Kwa maneno haya, tatizo langu limekwisha.”[YOHANA 10:10; 3 YOHANA 1:2] n.k.

Usiseme maneno kama yafuatayo, ukatengwa na kukamatwa na Shetani na kushindwa: “Labda nitapona”. “Mungu akipenda nipone, nitapona.” “Hali yangu imezidi kuwa mbaya baada ya maombi, nafikiri ugonjwa huu utaniua.” – Ukisema hivi, utakufa kweli, utapata matunda ya kinywa chako! Baada ya maombi, kiri maneno ya Mungu ya Ushindi bila kuangalia maumivu yanayoendelea au mazingira yanayokukabili wakati huo.

VIZUIZI KUMI VINAVYOFANYA MAMLAKA YAKO ISITENDE KAZI KUBWA

NA KUWEZA KUPATA MAJIBU YA MAOMBI KWA KIWANGO CHA JUU

Yesu alisema kwamba yeye amwaminiye, atazifanya kazi alizozifanya yeye na hata kubwa zaidi kuliko alizozifanya Yesu. [SOMA YOHANA 14:12]. Lakini leo utaona kwamba watu wengi wanaomwamini Yesu, wanasumbuliwa na kazi ndogo tu za Shetani na mamlaka yao inashindwa kutenda kazi. Viko vizuizi vinavyosababisha mtu asione miujiza mikubwa inayotokana na maombi na mamlaka yake juu ya Shetani:-

(1) Kutaka miujiza tu na ukawa hutaki kumfuata Yesu katika mambo yote

[MATHAYO 6:33; YOHANA 6:24-27; ZABURI 91:14-16].

(2) Yesu alikuwa chini ya amri ya Baba wakati wote. Baba alivyomwamuru ndivyo alivyofanya. [YOHANA 14:31]. Hii ndiyo iliyokuwa siri kubwa ya Yeye kutenda kazi kubwa na kuwa na mamlaka yote juu ya Shetani. Leo watu wengi waliookoka hawataki kuwa chini ya amri ya Baba yaani kufuata amri zote katika Neno la Mungu. Wanaongeza na kupunguza katika Neno la Mungu na kuchagua yale yaliyo rahisi kwao kuyafanya. Kufanya hivyo ni machukizo na kutafuta kupigwa na Shetani. [KUMBUKUMBU 4:2; 12:32; MITHALI 30:5-6; UFUNUO 22:18-19]. Kufanya yote aliyoamriwa, ndiyo ilikuwa siri ya Yoshua kufanya kazi kubwa na kuwa na mamlaka kuu juu ya Shetani. Alipoamuru Jua kusimama, lilitii. Siri ya ushindi huo, ni Yoshua kufanya YOTE aliyoamriwa na Mungu kupitia kwa Musa. [YOSHUA 11:15]. Ukitaka kuona mamlaka yako inatenda kazi kubwa, mtii aliyekupa mamlaka na kuyafanya yote anayokuamuru. Usiseme kufanya hili na hili siyo lazima. Usiseme kubatizwa katika maji tele baada ya kuamini siyo lazima; usiseme kutoa fungu la kumi katika mapato yako yote siyo lazima. Usiseme kuvaa mavazi ya kidunia na kufanana na mataifa siyo tatizo. Ukichagua ya kufanya, mamlaka yako inakuwa dhaifu sana. Hakikisha siku zote maisha yako yote yanakuwa sawa na HESABU 23:26. Siku zote wafukuze watenda mabaya wanaokushawishi kuacha kuyatenda maagizo yote ya Mungu [SOMA ZABURI 119:115].

(3) Kutafuta kuwapendeza wanadamu badala ya Mungu. Yesu siku zote

alihakikisha anafanya kila njia kumpendeza Mungu siku zote. Hii ndiyo siri nyingine ya nguvu yake ya maombi. [SOMA YOHANA 8:29]. Tatizo kubwa kwa watu wengi waliookoka, wanatafuta kuwapendeza wanadamu na kuonekana wazuri kwao, badala ya kutafuta kumpendeza Mungu. Mashujaa wote waliokuwa na uwezo mkubwa katika maombi yao, walikuwa wanatafuta kumpendeza Mungu kabla ya yeyote. Hii ndiyo iliyokuwa siri ya ushindi kwa Daudi na kuwa na uwezo wa kumpiga Goliathi kwa jiwe MOJA tu lililokuwa kwenye kombeo. [SOMA ZABURI 73:25].

(4) Kuigeukia miungu mingine. Kazi yako, biashara yako, mchumba wako, ndugu

zako, wazazi wako, masomo yako au vitu vyako vinaweza kuwa ni miungu yako ikiwa vinakufanya ukose nafasi ya kumwabudu Mungu, kufanya kazi yake, na kuwa na usharika naye. Jambo hili husababisha uso wa Mungu ufichwe kwako, na usione majibu ya maombi. [SOMA KUMBUKUMBU 31:18].

(5) Ikiwa viungo vyako vya mwili vinatumika kutenda dhambi, Mungu anapoviangalia, anaviona vimejaa damu na uchafu. Vidole vinavyoshika sigara, mikono inayotumika kushika bia, midomo inayotumika kusema uongo na kusengenya, miguu na viuno vinavyotumika kucheza Disco na Ngoma, viungo vyako vya siri vinavyotumika kufanya uasherati na uzinzi, macho yako yanayotumika kuangalia sinema na video za kidunia, masikio yako yanayojistarehesha kwa kusikia miziki ya kidunia katika radio n.k. Kila kiungo kinachotumika kutenda dhambi, mbele za Mungu kinakuwa kimejaa damu na uchafu na kinafanya uso wa Mungu ufichwe kwako na usione majibu ya maombi kwa kiwango cha juu [SOMA ISAYA 1:15; EZEKIELI 39:24; ISAYA 59:2-3].

(6) Kutokuwa tayari kujifunza Neno la Mungu na kulitenda. Wako watu wengi waliookoka ambao baada ya kuokoka, hawaoni umuhimu wa kutafuta mafundisho kwa bidii bali wanazunguka huko na huko kutafuta mikutano ya Injili tu. Baada ya kuokolewa, hupaswi kutafuta Injili ya kukuokoa tena! Inakupasa kutafuta mafundisho au maarifa. Ukichukia maarifa, majibu ya maombi yako yanakuwa hafifu [SOMA MITHALI 1:28]. Yesu alinena kama Baba ALIVYOMFUNDISHA [ANGALIA YOHANA 8:29]. Ikiwa Yesu alikubali kufundishwa, ni zaidi sana sisi. Hiyo ndiyo iliyokuwa siri ya ushindi wake na kwa unyenyekevu anatuonyesha siri hiyo. Unapokubali kutafuta mafundisho ya KWELI hata yakiwa magumu namna gani, ujue kweli hiyo ndiyo itakayokuweka huru wakati wote. Maneno ya Mungu yakiwa kwa wingi ndani yako, majibu ya maombi yako yatakuwa dhahiri. [SOMA YOHANA 8:31; YOHANA 15:7]. Kumbuka pia kwamba kulijua Neno la Mungu bila kulitenda ni kuwa sawa na Shetani. Yeye analijua Neno la Mungu lakini halitendi. Ili uwe tofauti na yeye na kumshinda kwa mamlaka, sikiliza lolote katika neno na kulitenda au siyo, utalia na usisikilizwe na BWANA (SOMA KUMBUKUMBU 1:43, 45).

(7) Mashaka kabla au baada ya maombi, huzuia kabisa majibu ya maombi. Bila mashaka au kusitasita, mwendee Mungu ukijua hakika atafanya. [SOMA YAKOBO 1:6-7; WAEBRANIA 10:38; MARKO 11:23].

(8) Makusudi yako ya maombi ni lazima yawe ya kupata na kulitumia jibu kwa

utukufu wa Mungu na siyo kwa tamaa tu! [YAKOBO 4:3; 1 WAKORINTHO 10:31].

(9) Kumpiga mkeo, kutompa heshima na kumuonea tu kwa kuwa ni chombo

kisicho na nguvu; jambo hili husababisha pia maombi yako kuzuiliwa na kutopata majibu[SOMA 1 PETRO 3:7].

(10) Kutohubiri Injili kwa watu ambao hawajaokoka pia husababisha mamlaka yako

kupungua na majibu yako ya maombi kuwa mbali. Watu ambao hawajaokoka ni maskini wanaohitaji habari njema. Yesu aliwahubiria maskini hawa habari njema. Ukiziba masikio usisikie kilio chao cha kutaka habari njema, na kuwaacha waende Jehanum, wewe pia maombi yako hayatasikiwa [SOMA MITHALI 21:13]

Ukikaa katika mafundisho haya, utajua kwamba Mungu wetu yuko karibu mno na anajibu kila tumwitapo [SOMA KUMBUKUMBU LA TORATI 4:7]. - See more at: http://www.gospelkitaa.co.tz/2014/06/somo-jinsi-ya-kuomba-mwenyewe-na-kupata.html#sthash.gHh3IFml.dpuf




Anatoli Levitini, mwandishi na mwanahistoria wa Kirusi, alitumia miaka yake mingi katika Gulag ya Siberia, ambako dua zilizotolewa kwa Mungu zilionekana kana kwamba zimeganda ardhini. Lakini alirudi akiwa mzima kiroho. "Mwujiza mkuu kuliko yote ni maombi," aliandika. "Yanipasa tu kumgeukia Mungu kimawazo na mara moja naisikia nguvu inayoingia ndani yangu kutoka mahali fulani, inaingia katika roho yangu, na mwili wangu wote. Je! hicho ni kitu gani? Je, naweza kuipata wapi hiyo nguvu inifanyayo mimi kuwa mtu mpya na kuniokoa mimi, niliye mzee duni sana, niliyechoka na maisha, ambayo itaniinua juu ya dunia hii? Inatoka nje yangu - wala hakuna nguvu yo yote ulimwenguni humu ambyo ingeweza kuipinga."
Katika mwongozo huu tunaona jinsi maombi yanavyotusaidia kujenga uhusiano wenye nguvu zaidi pamoja na maisha ya Kikristo yenye nguvu.
1. Kuzungumza Na Mungu
Je, tunawezaje kuwa na uhakika kwamba Mungu anatusikia tunapoomba?
"Ndipo mtaniita mimi na kwenda KUNIOMBA, nami NITA SIKILIZA. Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote." - Yeremia 29:12,13.

Je, ni uthibitisho gani aliotoa Yesu kuonyesha kwamba atasikia na kujibu maombi yetu?
"Basi nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, na mlango utafunguliwa kwenu." - Luka 11:9.

Maombi ni maongezi ya pande mbili. Hii ndiyo maana Yesu anaahidi anasema:
"Tazama nasimama mlangoni, nabisha. Mtu ye yote akiisikia sauti yangu, na kuufungua malngo, nitaingia na kula pamoja naye, na yeye pamoja nami." - Ufunuo 3:20.
Kwa jinsi gani inawezekana kwetu kuketi na kuwa na maongezi mazuri wakati wa chakula cha jioni pamoja na Kristo? Kwanza, kwa kumwambia kila kitu tulicho nacho moyoni mwetu kwa njia ya maombi. Pili, kwa kusikiliza kwa makini. Tunapotafakari wakati wa maombi, Mungu anaweza kuongea nasi moja kwa moja. Na tunapolisoma Neno la Mungu kwa roho ya ibada, Mungu ataweza kuongea nasi kupitia katika kurasa zake.
Maombi yanaweza kuwa njia ya maisha kwa Mkristo.
"OMBENI BILA KUKOMA; shukuruni kwa kila jambo, maana hayo ndiyo mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu." - 1 Wathesalonike 5:16-18.
Je! sisi tunawezaje "kuomba bila kukoma?" Je, yatupasa kupiga magoti wakati wote au kurudia-rudia kusema maneno ya kumsifu au kutoa dua? La, hasha. Lakini tunapaswa kuishi karibu sana na Yesu kiasi cha kujisikia huru kusema naye wakati wo wote, na mahali po pote.
"Tukiwa katika makundi ya watu mitaani, katika shughuli ya kibiashara, tunaweza kutoa dua yetu kwa Mungu na kumsihi atupe uongozi wake… Daima tungeacha wazi mlango wa moyo wetu na kuuacha mwaliko wetu ukipanda juu ili Yesu aweze kuja moyoni mwetu na kukaa humo kama mgeni wetu wa mbinguni." - Steps to Christ, uk. 99.
Mojawapo ya njia bora sana ili kujenga uhusiano huo wa karibu sana ni kujifunza kutafakari wakati tunapoomba.
"Kutafakari kwangu na kumpendeze yeye, mimi ninapomfurahia BWANA." -Zaburi 104:34.
Unapoomba usiharakishe tu kupitia orodha ya mambo unayotaka. Ngojea. Sikiliza. Kutafakari kidogo ukiwa katika maombi kunaweza kuuboresha sana uhusiano wako na Mungu.
"Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi." - Yakobo 4:8.
Kadri sisi tunavyozidi kumkaribia sana Yesu ndivyo kadri tunavyoweza kuonja kuwako kwake. Basi wewe unapaswa kuwa katika umbali wa kuweza kuongea na Yesu, wala usiwe na wasi wasi juu ya kusema maneno yaliyo sahihi. Ongea tu naye kwa unyofu wa moyo na bila kuficha kitu. Ongea juu ya kila kitu. Yeye amepitia maumivu makali sana ya kifo kile chenyewe ili apate kuwa Msiri wako.
2. Jinsi Ya Kuomba
Tunapoingia katika maombi, tunaweza kupenda kufuata muhtasari wa sala ya Bwana, sala ya mfano ambayo Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kuitikia ombi lao hili:
Tufundishe sisi kuomba.
"Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe, ufalme wako uje, mapenzi yako yatimizwe hapa duniani kama huko mbinguni. Utupe leo riziki yetu. Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tulivyowasamehe wadeni wetu. Wala usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu, kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina" - (Mathayo 6:9-13).

Kulingana na mfano huo ambao Yesu aliutoa katika sala yake, sisi tunatakiwa kumwendea Mungu kama Baba yetu aliye mbinguni. Tumwombe kwamba mapenzi yake yatawale mioyo yetu kama vile mapenzi yake yanavyotawala katika mbingu yote. Tunamtafuta ili atupatie mahitaji yetu ya kimwili, msamaha wake, kwa ajili ya kuwa na roho ya kuwasamehe wengine.
Kumbukeni ya kwamba uwezo wetu wa kuipinga dhambi unatoka kwa Mungu. Sala ya Kristo inahitimisha kwa maneno ya sifa kwake.
Safari nyingine Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kumwomba Baba "kwa jina langu" (Yohana 16:23) - yaani, kuomba kulingana na kanuni zake Yesu. Hii ndiyo maana Wakristo kwa kawaida hufunga sala zao kwa maneno haya: "Katika jina la Yesu, Amina." Amen (amina) ni neno la Kiebrania limaanishalo "Na iwe hivyo".
Japokuwa sala ya Bwana inatoa mwongozo juu ya mambo tunayotakiwa kuyaomba na jinsi ya kutunga sala, mawasiliano yetu na Mungu yanakuwa bora sana kama yanatoka moyoni mwetu kwa hiari.
Tunaweza kuomba juu ya kila kitu. Mungu anataka tumwombe msamaha kwa dhambi zetu (1Yohana 1:9), tumwombe atuongezee imani (Marko 9:24), tumwombe uponyaji wa maumivu na magonjwa yetu (Yakobo 5:15), na kumwagiwa kwa Roho (Zakaria 10:1). Yesu anatuthibitishia kwamba tunaweza kumpelekea yeye mahitaji yetu yote, pamoja na mashaka yetu; mno kuweza kumwomba.
("Mwekeeni matatizo yenu yote, maana yeye anawatunzeni") - 1 Petro 5:7.
Mwokozi wetu anapendezwa na mambo yo yote madogo yahusuyo maisha yetu. Moyo wake huchangamka wakati inapomwendea mioyo yetu kwa upendo na imani.
3. Maombi Ya Faragha
Wengi wetu tunayo mambo fulani ambayo tunasita kuwaambia hata marafiki zetu wa karibu sana. Kwa hiyo, Mungu anatualika sisi kuutua mzigo huo katika maombi yetu ya faragha: tukiwa kila mmoja peke yake na yeye. Si kwamba yeye anahitaji maelezo yote. Mwenyezi anajua vizuri sana kuliko sisi tunavyojua, makusudi yetu yaliyojificha moyoni mwetu, na chuki zetu zilizojificha ndani. Lakini tunahitaji kuifunua mioyo yetu kwake yeye atujuaye mpaka ndani kabisa, na atupendaye milele. Uponyaji unaweza kuanza Yesu anapoweza kuyagusa majeraha yetu.
Tuombapo, Yesu, Kuhani wetu Mkuu, yu karibu nasi kutusaidia:
"Tunaye mmoja ALIYEJARIBIWA KWA KILA NJIA, KAMA SISI TUNAVYOJARIBIWA -lakini alikuwa hana dhambi. Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupate kupokea rehema na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji" - (Waebrania 4:15,16).

Je, una wasi wasi, mfadhaiko, hatia? Weka hayo mbele zake Bwana. Ndipo yeye anaweza kukidhi kila hitaji tulilo nalo.
Je, ni lazima tuwe na mahali maalumu pa maombi hayo ya faragha?
"wewe unaposali, ingia katika chumba chako, funga mlango na kumwomba Baba yako, ambaye.. atakujazi." - Mathayo 6:6.

Zaidi ya kuomba wakati wa kutembea mitaani, kufanya kazi, au kufurahia mkutano fulani, kila Mkristo angekuwa na muda fulani uliotengwa kila siku kwa maombi yake yeye peke yake pamoja na kujifunza Biblia. Tunza miadi yako ya kila siku na Mungu wako wakati unapokuwa mchangamfu sana na wakati unapokuwa makini sana.
4. Maombi Ya Hadhara
Kujiunga pamoja na wengine katika maombi huwaunganisha watu kwa kifungo maalum na kukaribisha uweza wa Mungu kwa njia ya pekee.
"Kwa kuwa wawili au watatu wanapokusanyika pamoja katika jina langu, nipo pamoja nao pale." - Mathayo 18:20.
Mojawapo ya mambo makuu kuliko yote tuwezayo kufanya sisi kama familia ni kukuza maisha ya maombi ya pamoja. Waonyesheni watoto kwamba tunaweza kupeleka mahitaji yetu kwake moja kwa moja. Watakuwa na msisimko juu ya Mungu watakapoona anajibu maombi yanayohusu mambo halisi ya maisha yao. Ifanyeni ibada ya familia kuwa wakati wa furaha na kubadilishana uzoefu wa maisha katika hali ya uhuru.
5. Siri Saba Za Maombi Yanayojibiwa
Musa alipoomba, Bahari ya Shamu iligawanyika. Eliya alipoomba, moto ulishuka kutoka mbinguni. Danieli alipoomba, malaika aliyafumba makanwa ya simba wale wenye njaa kali. Biblia inatueleza visa vingi vya kusisimua vya maombi yaliyojibiwa. Tena inapendekeza kwetu maombi kama njia ya kupata ule uweza kwetu maombi kama njia ya kupata ule uweza mkuu wa Mungu. Yesu anaahidi hivi:
"Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nami nitalifanya" - (Yohana 14:14).

Lakini maombi mengine bado yanaonekana kana kwamba hayasikilizwi. Kwa nini? Hapa chini zipo kanuni saba zitakazokusaidia wewe kuomba kwa ufanisi zaidi:
(1) Uwe karibu sana na Kristo.
"NINYI MKIKAA NDANI YANGU, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtapewa." - Yohana 15:7.

Tunapoupa kipaumbele uhusiano wetu na Mungu na kuwa karibu naye, tutakuwa tunasikiliza na kutazamia kupata majibu kwa maombi yetu ambayo, vinginevyo, tusingeyatambua.
(2) Endelea Kumtumaini Mungu.
"MKIAMINI, mtapokea yote myaombayo katika sala zenu" - (Mathayo 21:22).

Kuamini au kuwa na imani, maana yake ni kwamba tunamtazamia Baba yetu aliye mbinguni kwamba kweli atatupa hayo mahitaji yetu. Kama wewe una wasiwasi kwamba huna imani, basi, kumbuka kwamba Mwokozi alitenda mwujiza kwa mtu yule aliyemsihi sana akiwa amekata tamaa, aliyesema:"
"Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu!" - (Marko 9:24).

Wewe kazana tu kuitumia imani ULIYO nayo; usiwe na waiswasi juu ya imani ile usiyo nayo.
(3) Jisalimishe kimya kimya chini ya mapenzi ya Mungu.
"Huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu cho chote SAWA SAWA NA MAPENZI YAKE, anatusikia" - (1 Yohana 5:14).

Kumbuka kwamba Mungu anataka kutufundisha sisi, pamoja na kutupa sisi vitu, kwa njia ya maombi. Kwa hiyo, wakati mwingine anatuelekeza upande mwingine. Maombi ni njia ya kutusogeza sisi zaidi na zaidi karibu na mapenzi ya Mungu. Hisia zetu zinatakiwa ziwe kali kutambua majibu ya Mungu na kujifunza kitu kutokana nayo. Kuyafuatilia kwa karibu maombi yetu fulani fulani ya pekee pamoja na kile kinachotokea kuhusiana nayo ni msaada mkubwa kwetu.
Roho Mtakatifu atakusaidia kulenga shabaha yenyewe: "Roho anawaombea watakatifu kulingana na mapenzi ya Mungu" (Warumi 8:27. Kumbuka kwamba mapenzi yetu yangeweza kulandana siku zote na mapenzi ya Mungu endapo sisi tungeweza kuona kama yeye anavyoona.
(4) Mngojee Mungu kwa Saburi.
"NALIMNGOJA BWANA KWA SABURI, akaniinamia akakisikia kilio changu" - (Zaburi 40:1).

Jambo kubwa hapo ni kukaza mawazo yako yote kwa Mungu, kukaza mawazo yako yote juu ya suluhisho lake. Wala usithubutu kumwomba Mungu akusaidie kwa dakika moja, na halafu kujaribu kuzizamisha shida zako kwa kujifurahisha katika anasa dakika inayofuata. Umngoje Bwana kwa saburi; tunahitaji kuwa na nidhamu hiyo vibaya sana.
(5) Usiing'ang'anie Dhambi iwayo yote.
("Kama ningalinuia maovu moyoni, Mwenyezi-Mungu hangalinisikiliza")- Zaburi 66:18.

Dhambi ijulikanayo hukata mara moja uweza wa Mungu katika maisha yetu; inatutenga mbali na Mungu (Isaya 59:1-2). Huwezi kuishika na kuing'ang'ania dhambi kwa mkono mmoja na kunyosha mkono mwingine kupokea msaada wa Mungu. Ungamo la dhambi litokalo moyoni hasa pamoja na toba ya kweli ndilo suluhisho la tatizo hilo.
Kama sisi hatutaki kumruhusu Mungu kutuweka huru mbali na mawazo, maneno na matendo yetu mabaya, basi, maombi yetu hayawezi kutuletea jibu lo lote.
"Hata mwaomba, wala hampati, kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu" - (Yakobo 4:3).
Mungu hatajibu "ndiyo" kwa maombi ya uchoyo. Acha wazi masikio yako yapate kuisikia sheria ya Mungu [Amri Kumi], yaani, mapenzi yake, naye ataacha masikio yake wazi kuzisikia dua zako.
"Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria [Amri Kumi], hata sala yake ni chukizo" - (Mithali 28:9).

(6) Tambua Kwamba Unamhitaji Mungu.
Mungu huwajibu wale wanaoomba kuwako kwake na uweza wake katika maisha yao.

"Heri wenye njaa na kiu ya haki, maana hao watashibishwa." - Mathayo 5:6.
(7) Kuendelea Kuomba Tu.
Yesu alitoa kielelezo cha kuwapo kwa haja ya kuendelea tu kutoa dua zetu kwa kusimulia kisa kile cha mjane aliyekuwa anaendelea tu kuomba na kuendelea kuja kwa hakimu akiwa na ombi lake lile, lile. Mwishowe yule hakimu alisema, huku akiwa ameudhika vibaya sana, "Kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitahakikisha kwamba nampatia haki yake." Kisha Yesu alitoa hitimisho lake hili: "Je! Mungu hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku? Je! atazidi kuahirisha kuwapatia haki yao?" (Luka 18:5-7).

Zungumza na Mungu juu ya mahitaji yako yote, matumaini yako yote, na ndoto zako zote. Omba mibaraka ya pekee, omba msaada unapokuwa na shida. Endelea kutafuta, tena endelea tu kusikiliza, mpaka ujifunze kitu fulani kutokana na jibu lake Mungu.
6. Malaika Wanayahudumia Mahitaji Ya Waombao
Mtunga Zaburi alishangilia kwamba kwa njia ya huduma ya malaika wa Bwana maombi yake yalijibiwa:
"Nalimtafuta BWANA akanijibu; akaniponya na hofu zangu zote... malaika wa BWANA hufanya kituo kuwazunguka wale wamchao na kuwaokoa" (Zaburi 34:4-7).

Tunapoomba, Mungu anawatuma malaika zake kujibu maombi yetu (Waebrania 1:14). Kila Mkristo anaye malaika wake mlinzi anayetembea pamoja naye:
"Angalieni msimdharau mmojawapo wa wadogo hawa. Kwa maana nawaambia ya kwamba MALAIKA WAO mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni." - Mathayo 18:10.

Kwa sababu ya maombi yetu tunayotoa:
"Bwana yu karibu. Msiwe na wasiwasi na jambo lo lote, lakini katika kila jambo kwa maombi na dua zetu pamoja na kushukuru, wekeni mambo yenu myatakayo mbele zake Mungu. Ndipo amani ya Mungu, ipitayo ufahamu wote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu." - Wafilipi 4:5-7.

7. Mtindo Wa Maisha Ya Kikristo
Biblia inaeleza wazi juu ya mtindo wa maisha ya Kikristo. Kulingana na Waefeso 4: 22-24, Mkristo anatakiwa ku"vua" mtindo wake wa maisha ya zamani uliotokana na "tamaa zenye kudanganya", na ku"vaa" mtindo mpya wa maisha ambao ume"umbwa kwa mfano wa Mungu." Katika maandiko hayo na mwongozo tuligundua kwamba wakati ule wa kuzaliwa upya sisi tuna"umbwa upya" kuwa watu tofauti ndani ya Kristo.
Mwongozo huu na miongozo sita inayofuata hutangaza upya mtindo wa maisha ya Mkristo; huifunua siri ya maisha ya Kikristo yenye furaha. Itakusaidia wewe kujenga uhusiano wenye nguvu zaidi na Kristo, ambao matokeo yake yatakuwa mtindo wa maisha ya Kikristo ulio tofauti. Kwa hiyo kaza macho yako kwa Yesu leo hii, nawe unaweza kuwa na sehemu katika sherehe ile ya mwisho ya ushindi wakati amani yake Kristo itakapotawala bila kupingwa.
MADA YA KWANZA.           MAHUBIRI.

Malengo ya mada.
Baada ya kumaliza mada hii mwanafunzi ataweza.
§  Kueleza maana yamahubiri.
§  Kueleza maana ya kuhubiri.
§  Kueleza wito wa kuhubiri ulivyo.
§  Kueleza umuhimu wa  kujifunza homiletics.

A. UTANGULIZI
Katika kozi hii tutashughulikia mojawapo ya kazi kuu ya kanisa.
Mojawapo ya wajibu mkuu ambao umewekwa mikononi mwa kanisa ni kuhubiri  ujumbe wa Mungu yaani Injili. 1Kor 1:21
a)      Ni amri iliyo wazi toka kwa Bwana Yesu kwa wafuasi wake. Mk 16:15.
                   “Enendeni ulimwenguni mwote mkaihibiri Injili kwa kila kiumbe”.

b)      Kuhubiri ni  mojawapo ya kazi ya thamani sana ambayo Mungu ametupa. Kuwa msemaji wa Mungu, yaani Mjumbe wa Kristo.  2Kor 5:20.
c)      Kuhubiri ni wajibu mkuu.  Rumi 10:14-15.
d)     K wa njia ya mahubiri Mungu  alichagua kujidhihirisha mwenyewe kwa mwanadamu.
 B. MAANA YA MAHUBIRI.
Neno mahubiri linatokana na maneno mawili ya kigiriki ambayo ni homileo na homilia yenye maana ya ‘kuwa pamoja na, kuongea na kuwasiliana.
a)      Homily pia humaanisha ujumbe au hotuba.
b)      Elimu inayohusu namna ya kuhubiri huitwa Homileticts.
c)      Homiletics ni ustadi wa kuhutubia au kuhubiri.
d)     Mtaalamu wa elimu ya kuhuri huitwa Homilist
e)      Homiletics huhusisha kujifunza kila kitu kinachohusiana na ujuzi wa kuhubiri au kutunga hotuba.
f)       Mahubiri huhusu kujifunza kila kitu kinachohusiana na ujuzi wa kuhubiri masomo ya Biblia.
g)      Mahubiri ni ujuzi wa kuhubiri.
h)      Ni elimu au taaluma inayohusu kuhubiri Neno la Mungu.
i)        Ni elimu inayohusu namna ya kuhubiri.{ somo juu ya kila kitu kinachohusiana na kuhubiri}.
j)  Kuhubiri ni kutangaza ujumbe wa Mungu. Mungu hutumia watu wake aliowachagua kuhubiri ujumbe wake.
     k)  Ujumbe unapaswa kuwa ujumbe wa Mungu Kitu kingine chochote na ujum
          si mahubiri ila ni maoni na falsafa za kibinadamu tu.
l) Kuhubiri ni lazima kuwe ni kutangaza binafsi na si kusoma au kuandika
a)      Dr. Martyn Lolyoyd Jones alisema  “ Wahubiri huzaliwa na hawafanywi kamwe. Kamwe hutamfundisha mtu kuwa mhubiri kama yeye si muhubiri. Lakini muhubiri wa kuzaliwa unaweza kumsaidia na kumwendeleza akawa mhubiri bora kwa njia ya mafunzo”
b)      -Mhubiri si chanzo cha ujumbe.Mungu ndiye chanzo cha ujumbe na mhubiri ni bomba au mfereji ambako Mungu hupitishia ujumbe wake kwenda kwa watu aliowakusudia. Ujumbe wa Mugu hutiririka kupitia utu wa  mhubiri.
c)      -Ujumbe unapaswa kutiririka kwa uhuru toka kwenye chanzo chake (Mungu) kwenda   kwa  wakusudiwa yaani hadhira au wasikilizaji.
d)     Mahubiri ni zao la mambo mawili  ambayo ni Mungu na mhubiri.Mahubiri mazuri huzaliwa kutokana na ushirikiano mzuri (umoja) na ushirika mzuri  kati ya Mungu na mhubiri.
Hivyo kuna vipengele viwili vya wazi katika mahubiri S cha kwanza ni kile cha ki Mungu na cha pili ni kile cha kibinadamu.
Kwa sababu ya wito wake mkuu mhubiri anapaswa kuwa mwaminifu na awe na  ufahamu wa kutosha juu ya Neno la Mungu.

C. MAANA YA KUHUBIRI.
Mahubiri yana lengo mahususi katika mpango wa Mungu.  Ni  njia mabayo kwayo Mungu ameamua kuwafikia waliopotea dhambini na kuwaimarisha waamini.Kkwa sababu mahubiri ni njia ya mungu  kuwafikia wanadamu tutatazama maana ya kuhubiri kwa mitazamo mbalimbali kama ilivyo ainishwa na wataalamu wa masomo ya homiletics.
1.Kuhubiri ni kuielezea imani.
Mojawapo ya malengo ya mahubiri ni kuelezea au kutangaza kweli za maandiko matakatifu. Kila hotuba au ujumbe wapaswa kuwasilisha kweli za maandiko kwa njia itakayowezesha hadhira kupata uelewa zaidi ju ya maandiko matakatifu.Kuhubiri husababisha imani kuumbika kwa wasikilizaji wako. Hubiri kwa kukuza imani na kuielezea imani katika mwana wa Mungu.
II. Kuhubiri ni kuitetea imani.
Haitoshi kuelezea ukweli wa Mungu bali tunapaswa kuutetea. Shetani, ulimwngu na maadui wa imani huvamia na kupotosha kweli za neno la Mungu. Hivyo ni lazima kwa mhubiri yoyote kuwa tayari kuitete imani ya kweli kwa njia ya kuhubiri kweli za ki-Biblia. Kuna wahubiri wengi wa uongo ambao kazi yao ni kuposha kwali za maandiko matakatifi. Ni jukumu la kila mhubiri wa kweli kuhakikisha anasimama imara katika kuitetea imani ya kweli.
III.Kuhubiri ni kuinjilisha.
Wajibu mkubwa wa Mhubiri ni kuitangaza injili kwa watu waliopotea dhambini. Ni lazima watu wote waliopotea wapelekewe injili ili wapte kutambua  hali yao ya kupotea na kuongozwa kwenye wokovu wa Yesu Kristo.
IV. Kuhubiri ni kukemea dhambi.
Kama ukichunguza hotuba za agano jipya utagundua kwaqmba hakuna mubiri hata mmoja aliyesita kukemea dhambi.mfano Yesu, Yohana, Paulo, Petro n.k wote walikemea dhambi kwa nguvu zo katika kila mahubiri. Mhubiri nilazima akemee dhambi kila mara kwani Mhubiri ni kinywa cha Mungu. Kemea dhambi bila kuogopa chochote .
V. Kuhubiri ni kuhamasisha waamini.
Mahubiri hutakiwa kuwasaidia wakristo kukua katika neema ya Mungu. Pamoja na kuonya na kukemea dhambi mahubiri hutakiwa kuwahamasisha na kuwawezesha waaamini kukua kiroho na kufikia kimo cha Kristo.
VI. Kuhubiri ni kufikia mahitaji ya hadhira.
Mahubiri yatakuwa yameafanikiwa kama yatakuwa yamepokelewa na kukutana na mahitaji ya waikilizaji. Mhubiri kwa uangalifu anatakiwa kujiweka katika daraja sawa na wasikilizaji. Anatakiwa kujitahidi kuhakikisha unapokelewa na makutano na kukutana na mahitaji yao.
VII.Kuhubiri ni kudhihirisha uweza wa Mungu. Bwana Yesu aliahidi  kuwa na wahubiri kwa kulithibitisha neno kwa ishara na maajabu. Popote injili inapohubiriwa ni sharti Bwana awepo
akiithibitisha kwa isharaMk 16:15,20. 1Kor 2:4

 D.  WITO WA KUHUBIRI
Sehemu ya muhimu sana katika kuhubiri ni wito. Kimsingi wito ni wa mtu binafsi Mungu huwaita watu katika huduma na watu hupokea hilo  rohoni mwao kisha huja uthibitisho wa nje kupitia kanisa au watumishi mbalimbali na fursa mbalimbali. Mungu Huwaita watu wake katika nafasi na huduma mbalimbali. Wengine kuwa wachungaji, wamishenari, wazee wa kanisani, wainjilisti, au huduma nyinginezo.
Kazi ya kuhubiri si ajira ambayo mtu anakwenda chuoni kusoma kwa lengo la kupata  baada ya kuhitimu masomo yake, bali ni mwito mtakatifu ambao mtu huitwa na Mungu mwenyewe kuwa muhubiri.
  Mtu huenda chuoni ili kupata maarifa yatakayomwezesha na kumsaidia katika kutimiza mwito wa Mungu uliondani yake. Haendi chuoni kupata mwito bali wito husababisha mtu kwenda chuoni  kama sehemu ya maandalio.
Hivyo wito usichanganywe na ajira na maslahi binafsi ya mtu. Ni lazima wito uheshimiwe na kuogopwa. Waamini hawapaswi kujihusisha na huduma kwa lengo la kujinufaisha na kujipatia mali kwa njia za ujanja ujanja.
Kimsingi kila mwamini ni muhubiri kwani agizo kuu linamhusu kila mwamini. Kila mwamini anapaswa kujihusisha na kupeleka injili kwa watu waliopotea dhambini hili ni agazo la jumla.
Lakini kuna watu maalum  ambao Bwana ameweka wito wa muda wote(Full time commitement) ndani yao. Amewachagua kwa kusudi hili katika maisha yao na muda wao wote. Hawa wanasimama katika zile huduma tano za uonozi katika kanisa, ambao ni mitume,  manabii,  wainjilisti, wachungaji na waalimu. Hawa ndio Bwana amewaweka kusimama katika kazi ya kuhubiri ya muda wote, Wao hawapaswi kujihusisha na shughuli zingine bali kazi yao ni kulihudumia Neno na kuomba yaani Kuhubiri. Bwana ameweka mwito mtakatifu ndani yao ambao ni wajibu mkuu na wa kuogofyapia{.Mdo6:2,4} hili ni agizo mahususi.
Wito huu haupatikani kwa njia ya kusoma au kwa njia ya ulaghai bali kwa kuitwa na Mungu mwenyewe kuwa msemaji wake. Kuna baadhi ya makanisa ambayo yameufanya wito wa Mungu kuwa ni ajira. Kwani wao huwapeleka watu kwenda chuoni kusomea huduma fulani mfano uinjilisti, uchungaji nakadharika kwao wito si jambo la msingi ila elimu  ndiyo yenye kupewa kipaumbele. Wao humpa mtu kushika  nafasi ya huduma baada ya kuhitimu mafunzoya chuo cha Biblia bila kujali kama ana wito au la.
Matokeo yake ni kwamba makanisa yamekuwa yakiongozwa na kuhudumiwa na watu wasio na wito wenye kutegemea elimu ya darasani tu, jambo ambalo ni hatari kwa maendeleo na uhai wa kanisa.
Elimu ni jambo la zuri sana lakini elimu haiwezi kuchukua nafasi ya wito katika kanisa la Mungu ikiwa tunataka kufikia kusudi la Mungu la mwito mtakatifu na kusimama kiuaminifu mbele zake kupata ushindi mkuu.
Usiwe mtumwa wa elimu.  Elimu hii unayopata ikusaidie katika kumtumikia Mungu na kufanya huduma lakini isichukue nafasi ya Roho mtakatifu katika maisha yako na huduma yako. Wala haipaswi kuwa badala ya Roho mtakatifu.
Usiongozwe na elimu bali ongozwa na Roho mtkatifu.
Usihubiri kwa maneno yenye hekima pekee kwa lengo la kushawishi akili za watu bali hubiri  Kwa dalili za Roho mtakatifu na  nguvu. 1Kor 2:4.
Hakikisha unautumikia wito ambao Mungu ameweka ndani yako kwa gharama yoyte ile bila kujali mazingira au kitu kingine chochote.
Kwa hiyo wito wa kuhubiri  hautoki kwa mwanadamu yoyote Yule bali toka kwa Mungu mwenyewe. Mungu huwafanya watu wake kuwa wahubiri.
Jiulize wewe ni mhubiri wa kufanywa na nani ?
Kweli kuu kuhusu wito wa kuwa mhubiri.
1. Roho mtakatifu huweka wito ndani ya mtu.
 Wito wa Mungu huja juu ya mtu kupitia Roho mtakatifu. Katika akili ya kawida ni kazi kubwa kuhubiri au kutumika. Wito huja kwa watu wa aina zote na umri wote wowote. Baahi ya watu husikia wito na kujitoa wangali wadogo lakini wengine katika umri mkubwa n.k

2. Shauku ya  kutimiza wito.
Watu wanaoitwa kuwa wahubiri waliumbwa na Mungu kwa kusudi hiloYer1:4-10
Hawawezi kupata utoshelevu kwa kufanya kitu kingine chochote. Hawawezi kupinga kujihusisha katika huduma au kuchukua fursaza kuhubiri. hHata kama hakuna nafai za kutumika moja kwa moja  bado watatafuta nafasi katika huduma yoyote inayojitokeza.
3. Mungu huwaandaa wale anaowaita kwajili ya huduma.
Mungu hawaiti watu ambao hwana uwezo wa kutimiza mwito wake. Wahubiri wengi wanakipaji cha kuongea. Watu wenye wito juu ya watoto hupewa  hupewa Mungu huwaandaa kwa kuwapa uwezo kwa kufanya huduma na watoto n na wanaoitwa kuwa wacghungaji huqwezeshwa kuwa wachungaji. Popotye na kwa namna yoyte Mungu huwaandaa na kutoas nguvu ya uwezesho juuv yao.


4. Wito wa Mungu wapaswakuwa wazi.
Wito wa Mungu usifichwe. Wito wa Mungu ulioju yako wapaswa kuwa wazi kwa watu wangine lakini haupaswi kukimbilia kwenye wito huo mara moja. Hutakuwa na furaha na mafanikio na wito huo mpaka utakopokuwa umejisalimisha kwa mapenzi sahihi ya Mungu juu yako.
5. Wito wa Mungu ni wito wa matayarisho.
Kuna wajibu mwingi na mkubwa ambao huja pamoja na wito wa kuhubiri .Mungu akisha mwita mtu humuandaa kwanza kabla ya kumtuma na kumwachilia kwnye huduma aliyomuitia. Mhubiri anapaswa kujiimalisha kiroho na kimwenendo.Anatakiwa ajiandae kiakili kwa kusoma na kupata mafunzo. Pia anapaswa kujiandaa kimatendo kwa kunuo vipawa vilivyondani yake na kuyatisha maisha yake yote kulingana na wito ulio ndani ya
E.Umhuhimu wa kujifunza somo hili la homiletics.
a)      Linatusaidia kujua mbinu mbalimbali za kuhubiri.
b)      Linatusaidia jinsi ya kuhubiri bila kuwachosha watu.
c)      Linatufanya kuwa na ujasiri tunapohubiri.
d)     Linatusaidia kuhubiri kwa usahhi.
e)      Linatusaidia kutambua mahubiri ya uongo.
f)       Linatusaidia kujua nakuheshimu wito tulio nao.
g)      Linatusaidia kujua kusudi la Mungu la mahubiri.




                            Zoezi.
Jibu maswali fafuatayo. Wanafunzi waweza kujibu katika makundi au mmoja mmoja kama kazi ya nyumbani kwa kadri mwalimu atakavyoona inafaa.

1. eleza maana ya  mahubi kwa mitazamo mbalimbali.
2.Eleza vile mahubiri yasivyo.
3. Toa tofauti iliyopo kati ya mahubiri na kuhubiri.
4. Taja faida tano za kujifunza somo la kuandaa mahubiri.
5. Tathmini misukumo mbalimbali inayosababisha watu waingie katika huduma tano za uongozi wa kanisa. na hali hawana wito.
6.Eleza namna gani mtu aweza kujua kwamba Mungu anamwita kuingia katika huduma.
7.Eleza umuhimu wa kindicha maandalizi na matayarisho kabla yam tub kuingia katika huduma ambayo Mungu anamwita kuifanya.
8. Jadili kauli inayosema wito wa Mungu ni wito wa matayarisho.
9. jadili usemi unaosema kwamba Mungu humuanda mtu aliyemwita kabla ya kumwachilia katika huduma.
10. Jadili mabo ya msingi kuzingatia katika kipindi cha matayarisho  kwajili ya huduma  na wito ambao Mungu ameweka ndani yako.



MADA YA TATU:         MBINU ZA UTAYARISHAJI WA MAHUBIRI.

Utngulizi
Katika mada hii tutajadili aina mbalimbaliza utayarishaji wa mahubiri, maeno ya mahubiri na sehumu za mahubiri au hotuba. Tutapitia kwa undani kla kimojawapo ili kujifunza jinsi vipengele hivyo jinsi vinavyohusiana na amhubiri tunavyoweza kuvitumia katika huduma ya kuhubiri na kuandaa mahubiri.

Malengo ya mada.
Baada ya kumaliza kujifunza mada hii  mwanafunzi ataweza.
Kutambua njia na mbinu mbalimbaliza utayarishaji wa ujmbe au hotuba.
Kuandaa mahubiri kwa kutmia mbinu mbalimbali.
Kutambua sehemu tatu za mahubiri au hotuba.


A.  Utayarishaji Wa Somo.

Kuna aina nyingi za utayarishaji wa somo au hotuba, na kila mojawapo ina umuhimu wake. Lakini katika mada hii tutajifunza aina tatu za utayarishaji wa somo au hotuba.
Kila mwanafunzi anatakiwa kuelewa aina zota tatu na anapaswa  kujizoeza kutumia njia hizi zote ili aweze kufaidika zaidi.

1. SOMO LILILOANDIKWA.
Katika aina hii mhubiri hupaswa kuandika ila kitu anachokusudia kukihubiri. Wakati mwingine  somo lote huandikwa. Kilac eneo la asomo huchambuliwa kwa undani na kuwekwa katika maandishi. Ujumbe au somo lote huandikwa kikamilifu kabla ya kuhubiri.
Mhubiri huelezea kwa undani somo lake anapohubiri likiwa katika maandishi. Mhubiri anapohubiri mara nyingi hupitia kila kitu alichokiweka katika maandishi.

Faida za aina mbinu hii.
a)      Ujumbe wote huandaliwa kwa uangalifu mkubwa.
b)      Ujumbe huwasilishwa kwa umakini na uhalisia.
c)      Ujumbe huwa ni wa kitaalam.
d)     Mhubiri  hujikita katika somo.


Hasara ya mbinu hii.
a)      Somo huwa haliwavutii wasikilizaji.
b)      Utoaji wa ujumbe wa namna hii unaweza kuwa wa kuchosha usipofanywa kwa uangalifu.
c)      Utayarishaji wake huhitaji muda mwingi.

2.SOMO LISILOANDIKWA.
Hii ni mbinu ya utayarishaji wa somo bila kuliandika. Mhubiri huosma vifungu vya maandiko na kivitafakari kwa kina kisha hukariri vitu vya msingi vilivyo katika ujumbe wake na maandiko yanayohusika.
Aina hii mara nyingi hutumika katika kutayarisha na kuhubiri ujumbe wenye uvuvio zaidi. Ujumbe hutiririka toka rohoni na huwa wa kuvutia mno.
Faidaza mbinu hii.
a)      Ni rahisi kutmia.
b)      Haihitaji muda mwingi wa matayarisho.
c)      Mhubiri huwa huru kutoa kila kinachokuja ndani yake maadam kinaendana na ujumbe wa somo.
d)     Huwasisimua wasikilizaji na kuwavutia.
Udhaifu wa mbinu hii.
a)      Mhubiri kutoka nje ya ujumbe wake hasa ikifanywa na mhubiri asiye na uzoefu.
b)      Wasikilizaji waweza kulielewa somo vibaya.  (waweza kuelewa vile somo lisichomaanisha).
c)      Somo kutowajenga wasilizaji na kuishia kusisimua tu akili zao.
d)     Somo kutokuwa na maana halisi na hivyo kutowajenga wasikilizaji.

3.MBINU YA SKELETONI.
Njia hii huhusisha kuandika maelezo ya somo au ujumbe kwa kifupi kwa lengo la kufanikisha utunzaji wa kumbukumbu sahihi  juu  ya ujumbe au somo.
Kwa maana nyingine ni kwamba mhubiri hutayarisha muhtasari wa ujumbe au somo.Mhutasari huo huwa kama skeleton ya somo mfano wa fuvu la binadamu.

Mhubiri huhubiri kwa kutumia skeleton hiyo. Kazi yake hasa ni kuweka nyama katika skeleton hiyo kwa njia ya mahubiri. Hivyo anapohubiri huweka nyama katika mahubiri yake ili yawze kuwa kitu kamili
. Mhutasari wa somo huwa kama mifupa ya ujumbe. Ndiyo mifupa mabayo huleta sura na mategemeo kwa kile mhubiri anachotamani kusema. Anavyosema anaweka nyama katika mifupa na kuufanya mwili wa somo lake. Hupanua mawazo yake ambayo maelezo yake  mafupi yamekuza.
Faida za mbinnu hii.
a)      Mbinu hii humpa mhuburi uhuruzaidi.
b)      Utoaji wa somo huwa wa kuvutia sana.
c)      Somo huwajenga wasikilizaji bila kuwachosha.
d)     Mhubiri huweza kutoa somo kwqa mtiririko mzuri na sahihi.

Maeneo  ya mahubiri.
Kuna maeneo makuu manne ambyo mahubiri huhusisha. Mhubiri yoyote ni lazima azingatie maeneo hayo ili aweze kufanikisha mahubiri yake.
I.Wazo
. Hii huhusu namna ya kupokea kichwa cha somo au ujmbe. Ni ujuzi unaohusu namna ya kupokea ujumbe toka kwa Mungu. Huhusu namna ya kuptata wazo la  awali na kichwa cha somo.
Mugu hupanda mbeguya wazo kuhusu somo au ujumbe siku kadhaa kabla ya mahubiri. Mbegu hiyo kukua kwa njia ya kuitafakari na maombi zaidi. Kutokana na ujuzi mhubiri aweza  kuuujenga uwezo wa kumbua mstari.
Muhubiri hupaswa kuliemneleza na kulikuza wazo lililopandwa ndai yake kwa njia ya maombi, kutafakari na kuchunguza zaidi juu ya wazo hilo ili aweze kutayarisha ujumbe.
Pata muda wa utulivu utulie uweponi na omba nuru zaidi ya ufunuo huo.

II.Muundo.
Muundo huhusisha uchambuzi wa  wazo ili kuweza kugundua kweli zilizomo katika wazo hilo.Baada ya kupokea Wazo toka kwa Mungu unapaswa uanze kulichambua ili  kutambua vitu ambavyo wazo hilo linavyo.
Katika hatua hii inapaswa kuorodhesha kwa urahisi kila kitu kilichomo kwenye wazo hilo.Mara nyingi unapokuwa katka hatua hii unahitaji kuandikwa kwa haraka ili kupata kwa kifupi mtririko wa uvuvio unaokuja. Hakikisha kwamba unaaandika kila kitu. Ili uweze kuchambua baadae.



Ujenzi.
Huhusiha kukusaya na kuayaweka mawazo yako uliyoyachambua katika kipengele cha uchambuzi katika mpango mzuri. Kuweka kila kitu katika mpangilio mzuri kutakusaidia na kukurahisishia katika utoaji wa somo lako.  Kuwasislisha mawazo yaliyoendelezwa hufanyika msaada sana kwa wasikilizaji wako katika kuelewa na kufuata mpango wako wa kufikiri.
Somo likiwalimechanganywa itawawia vigumu wasikilizaji wako katika kulielewa somo hilo.Ujenzi wa osmo hulenga kulifanya somo rahisi kiasi cha kueleweka vizuiri na wasikilizaji.
Ni muhimu sana kwa mhubiri kuliweka somo katika namna  itakayofanya lieleweke kwa urahisi.

Mawasiliano.
Hii huhusu namana  mhubiri anavyowaislisha somo au ujmbe kwa hadhira.  Mhubiri anatakiwa kuliwasilisha somo lake kwa njia rahisi na nyepesi kueleweka na waikilizaji wake. Anatak

a)      Kuwasilisha ukweli uliowazi na wenye kueleweka.
b)      Kuota ujumbe kwa njia ya kuteka akili za hadhira.
c)      Kuendeleza mawazoyako katika mpango ambao hadhira wataweza kuyafuata kwa urahisi.
d)     Kuwahamasisha hadhira  kulitendea kazi somo.  Yak 1:22.


B.  Sehemmu Kuu za Mahubiri na Hotuba.
Kwa kawaida mahubiri au hotuba yoyote ile ni lazima iwe na sehemtu tatu ambazo kwa pamoja huunda hotuba au mahubiri hayo.
 Sehemu tatu hizo ni utangulizi, kiini na hitimisho.Kila sehemu ni muhimusana na inatikwa kupewa uzito wake.
Sehemu mojawapo ikipuzwa yawza kuvuruga au kuharibu kabisa ujumbe au hotuba yako.
I. Utangulizi
. Hii ni sehemu ya kwanza ya hotuba. Utangulizi hutambulisha hotbuba au somo zima na kutoa picha jinsi somo litakavyokuwa. Utangulizi ni sehemu muhimu ya ujmbe na kama hadhira hawajakusikilza kwa umakini katika kipindi hiki cha awali yawezekana kutokuuelewa ujmbe wako au kutokukusikiliza vizuri katika sehemu zinazobaki za hotuba yako.
Mara nygingi utangulizi huwa kama muhtasari wa ujumbe.Katika utangulizi mhubiri huwaeleza hadhira kwa kifupi juu ya kile ulichopanga kuongelea au kuhubiri.

Mambo ya msingi katika uangulizi.
a)      Kuteka usikivu.  utangulizi wako unapaswa utawale hamu na mawazo ya wasikilizaji.

b)      Kujenga masikilizano. Lazima ujenge mawasiliano kati yako na wasikilizaji.

c)      Kuleta kukubalika. Ni lazima utangulizi kwako ukujengee kukubalika kwa wasikilizaji.
a.       Unapaswa kupata usikivu wao, matumaini na heshima. 

d)     Kujulisha.  Utangulizi wako unapaswa kuwaeleza wasikilizaji kwamba somo lako lina husu nini hasa, na jinsi utakavyoliwasilisha.

e)      Kusadikisha.  Ni lazima utangulizi uwasadikishe wasilizaji juu ya umuhimu wa ujumbe na kupata usikivu mzuri wa sehemu iliyobaki ya hotuba yako.
f)       Usitoe utangulizi kwa kuomba msamaha. Usiseme “Bahati mbaya sikujiandaa vizuri”
a.       Kufanya hivyo kutapoteza usikivu wa wasikilizaji wako na kukufanya usiaminike kwao.

Sifa za utangulizi mzuri.
a)      Sio wa kishindo mno. Utangulizi  uwe wa kiasi usiweke hatua ambayo huwezi kuifikia.
b)     Sio mrefu mno. Kumbuka kwamba utangulizi si ujumbe wote bali ni sehemu tu hivyo unapaswa kuwa mfupi.
c)      Utangulizi uendane na ujumbe. Utangulizi ni sharti ulenge kichwa cha somo. Waweza kuwa mhtasari wa somo au kisa  ambacho kinaonesha ukweli wakile ulichokusudia kuongelea.

d)     Unapaswa kuandaliwa kwa uangalifu. Kwa sababu utangulizi wako ni kitu muhimu katika kuvuta usikivu wa hadhira unapaswa kuandaliwa kwa umakini sana.
Tayarisha utangulizi wako kwa kujiuliza maswali yafuatayo
a)        Ningekuwa ni msikilizaji  ujmbe huu nini kingenitvuta zaidi ili kuleta usikivu katika yote niliyokusudia kuyasema?
b)     “ Ni jambo gani hasa ambalo lngekaata usikivu wangu?
Majibu yake unayoyapata ndiyo waweza kuyatumiak katika sehemu ya utangulizi wa ujumbe wako.
Utoe nafasi ya kuptia kwenye kiini cha ujumbe. Utangulizi unapaswa kutoa njia ya kupitia kwenda kwenye kiini cha ujumbe. Kusiwe na pengo kati ya utangulizi na kiini cha ujumbe.

2.Kiini.
 Hiini sehemu kuu ya somo au ujmbe ambayo imebeba ukweli wote wa somo. Hatua ya kwaza kwenye kiini ni kutoa sekeletoni ya kiini  na kisha hatua ya pili  ni kuweka nyama katika skeletoni yako.Waweza kuweka nyama katika sekeletoni yako kwa  kufanya yafuatayo:

Kufafanua  misamiati mbalimbali inayojitokeza kwenye kiini na kutoa maelezo ya dondoo ulizoziandaa. Tumia kamusi au itifaki ya Biblia katika kupata maana ya maneno hayo.

Kutumia vielelezso. Unapaswa kutumia vielelezo mbalimbali vitakavyosaidia katika kulielezea somo lako au ujmbe wako.
Waweza kutumia vielelezo vifuatavyo katika kulielezea na kufafanua ujumbe wako.
Vielelezo binafsi.
Wahusika mbalimbali katika Biblia  wanaoweza kutumika katika kuelezea dondoo zako. Ukweli wa kitaalam mfano sayansi,historia, uvumbuzi, Tiba. n.k
Hadithi zenye kufafanua somo lako.Usiwaachie hadhira kutoa fasili  ya bali ifafanue mwenyewe.

Unapaswa kukigawa kiini katika dondoo kwa kufuata mtiririko wa mawazo. Hubiri kwa kufuata mtiririko wa mawazo wa kimantiki.

3.Hitimisho.
 Hii ni sehemu ya mwisho ya hotuba au ujmbe lakini kipengele cha muhumi sana . Kipengele hiki kisipozingatiwa maana na malengo yote ya kuhubiri huvurugika na kutokuwa na maana. Hivyo ni lazima kipewe uzito unaostahili.
Mambo ya kuzingatia.
Tunia muda kidogo kwa kuuelezea ujmbe kwa kifupi. Kazia maeneo ya msingi unayofikiri kwamba hayakueleweka vizuri  kwa hadhira wakati ukuhubiri na yale yanayotakiwa kupewa uzito maalumu.
Pia waweza kurudia kuzitamka kwa sauti  dondoo za ujumbe wako kila moja.
Usiwachushe(bore)  kwa kuanza kurudia kuhubiri ujumbe wako wote.

Mwaliko. 
Mwaliko ni kipengele muhimu sana  katika hitimisho. Kwa sababu mahubiri ni tofauti na iana nyingine za hotuba hivyo mwaliko huwa ni muhimu sana kwa kuwa  mahubiri huhusu kuchukua maamuzi au hatua juu ya kile kilichohubiriwa. Mahubiri blia mwaliko huwa hayajafikia lengo la kuhubiri. Mwaliko ni lazima katika mahubiri ya aina yoyote ile.
Mwaliko huwa  ni wakati wa kuitikia  Kile Mungu amesema kupitia mahubiri. Ni wakati wa kutendea kazi kile kilichofundishwa au kuhubiriwa.

Mhubiri anapaswa kuufanya mwaliko kuwa wazi kwa wasikilizaji wote. Lengo la mwaliko si kuwaita watu madhabahuni tu bali ni kuwahamasisha watu kuweka ujumbe katika matendo. 
Pia Mhubiri hutakiwa kuuweka ujumbe wake katika matendo.

1.      Ukihubiri uponyaji waite watu madhabahuni na waombee uponyaji.
2.      Kuhubiri kutembea katika mamlaka unatakiwa udhihishe mamlaka hiyo.
3.      Ukihubiri utoaji waite watu kumtolea Mungu.
4.      Ukihibiri toba unapaswa kuwaongoza hadhira kwenye maombi ya toba na kuwaita madhabahuni wale wanohitaji kutengeneza kwa upya mwenendo na  mahusiano na Mungu na kuomba nao.
Wapeleke watu kwenye matendo na matumizi Mt 21:23. Yak 2:22.
Unatakiwa kuwaongoza hadhira  kuomba kwaajili ya ujumbe au somo kwa kadri ya maongozi ya Mungu na kwa kadri Mungu alivyosema na kila mmoja.
Unaweza kuwaongoza watu waimbe wimbo unaoendana na ujumbe uili kuwaogeza uweponi na kuwapa  hamasa.
Toa mwaliko kwa watu ambao wanataka kuokoka na kama wapo omba pamoja nao.

Baada ya hapo maliza na mkabiribishe anaehusika na ratiba inayofuata.
 Kwa kuhitimisha juu ya sehemu tatu za ujumbe au hotuba twaweza kuvifupisha vipenele vyote hivyo vitatu kwa sentensi tatu ambazo ni:

1.      Waambie hadhira kile unachotaka kuhubiri.(Utangulizi.)
2.      Hubiri kile ulichowaambia    (Kiini),     kisha:
3.      Waambie  kile ulichohubiri.(Hitimisho).

























    AINA MBALIMBALI  ZA MAHUBIRI.



I.  MAHUBIRI YA KIFUNGU.
 Aina hii ya mahubiri hujengwa juu ya kifungu kimoja kidogo  cha maandiko tu. Huhusisha  kuchagua maelezo fulani maalum ya maandiko na kuyachunguza, kuchambua na kugungua kweli zote zilizomo ndani yake na kuziwasilisha kwa waikilizaji kwa mtindo rahisi na wenye kueleweka.

A. Faida za mahubiri ya Kifungu.
a)      Huvutia.
b)      Huzuia kutoka nje ya somo.
c)      Hufanya mahubiri kuwa ya ki- Biblia.
d)     Humwongezea mhubiri ujasiri.
e)      Husaidia wasikilizaji kulikumbuka  somo.

        B.  Jinsi ya kuandaa mahubiri ya  kifungu.Kuna mambo kadha ambayo mhubiri anapaswa kuyazingatia wakati wa kuandaa mahibiri ya aya badhi ya mambo hayo yamejadiliwa hapa chini.

1.Soma Biblia mara kwa mara. Unapaswa kusoma Biblia mara kwa mara ikiwa unataka kuwa mhubiri mqwenye mafanikio katika huduma yako.
-Tenga muda wa kusoma biblia kila siku. Beba Biblia ndogo kila mahali unapokwenda ili upatapo mua uweze kuisoma.

2. Jifunze Biblia. Kujifunza ni zaidi ya kusoma.Kujifunza kuna husiha kusoma Biblia kwa undani kwa kuchunguza kikamilifu kila kitu kilicha katika maandiko unayosoma na kutafakari kwa kina,.Yos1:8.
Unapaswa kutafakari kwa uangalifu vitu unavyosoma. Viweke kwenye akiliyako na kuvifikiri tena na tena.
Unapaswa kujizoesha kuchambua kile ulichojifunza. Baada ya kukichambua kwa umakini unapaswa kukiweka tena akilini.
2. Kuwa na Daftari la kuandikia. Kila usomapo Biblia yako jitahidi kuwa na kalamu na daftari la kuandika mambo muhimu un ayo jifunza.Jenga mazoea ya kuandika kwa ufupikila ufunuo unaoupata.

3. Dumisha hali ya maombi.  Unapaswa kuwa katika hali ya maombi kila usomapo Biblia.Omba Mungu akufunulie upate kulielewa Neno lake.Pia unapaswa kumwomba  Mungu akupe usikivu juu ya kweli anazokufunulia katika Neno lake.


4. Jenga usikivu.Unapaswa kuwa katika hali ya utulivu na usikivu katika nyanjazote yaani kimwili, kiroho na kisaikolojia. Mungu hutoa  ufunuo wake kwa sauti ya kimya ndani ya roho ya mhibiri. Kama hunautulivu na usikivu wa kutosha ni vigumu kugundua   maarifa hayo..
-

C.Sifa za aya ya mahubiri
Kifungu cha mahubiri au aya yapasa kuwa  :

a. Yenye mamlaka ya ki-Biblia.  Mafundisho anayokusudia kuhubiri toka kifungu au                      aya fualni ya maandiko yapasa ikubaliane na ile biblia nzima inachofundisha.
Katika mahubiri ya kifungu kuna uwezekano wa kuchukua kimakosamstari nje ya maana yake na kuutumia kufundishia kitu ambacho Biblia haikubaliani nacho.

 Ni Muhimu sana kwa ,uhubiri kujua jinsi mstari anaoshughulikia jinsi unavyokubaliana na kusudi la sura yote na kitabu chote.
Daima mhubiri anapaswa kujitahidi kufasili aya yake katika  nuru ya yale ambayo Biblia nzima inafundisha.

b.Kamili.  Aya yapaswa kuwa katika maandisha ya ukweli ulio kamilika.
Baadhi ya wahubiri huchukua kifungu cha maneno katika mstari na kukitumia bila kujali maneno yaliyotangulia au yanayofuata. Jambo hili si zuri na huzaa mafundsho ya uongo. Na huku huitwa.  “Kulichanganya neno la Mungu na uongo……..2Kor 4:2.

Ni lazima uepuke jambo hili kwani litaleta kutokuaminika na maelezo yasiyo ya ki- Biblia na hatimae utawapotosha wasikilizaji wako.
c. Fupi kiasi. Kifungu cha mahubiri chapaswa kitolewe kwenye maelezo ya maandiko ambayo ni mafupi nay a kulizisha.
c. Ya kueleweka. Aya yapaswa kueleweka na iwe muhtasari wa kutosha wa kile unachotaka kukishirikisha.
*Unapaswa ubaki katika mipaka ya kile ambacho aya yako inaelezea.

D. Namna ya kuandaa mahibiri ya aya.
a. Elewa maneno yake vema.Kipitie kifungu kwa kukisoma mara kadhaa, kitafakari na kujenga kumbukumbu juu yake na kiseme mwenyewe kwako. Hakikisha unakielewa vizuri.
b. Elewa lugha yake.Tamabua lugha yake kama ina maana halisi au kama ni lugha ya mifanotu.
Jiulize kama mwandishi alikuwa na maana  hasaya kile alichokiandika au  maneno yake yachukuliwe kama mfano wa mahubiri?

c.Changanua ujumbe wake.Chambua uhjumbe unaoupata na kuutenga katika sehemu kadhaa zenye kulandana ili uweze kuuwasilisha kwa mtiririko mzuri.
d. Chunguza maneno yake. Jitahidi kugundua kile maneno hayo yalikusudia kuwasilisha hapo awali. Ikiwa una kamusi ya kigiriki au Kiebrania unapaswa kulitazama neno hilo kwa lugha ya zamani au Kigiriki. Jaribi kubaini kama kuna maana maalumu ndani ya mneno unalolishughulikia. 
Kufanya hivyo kutakusaidia kugundua maaana yoyote maalumu ambayo mwandishi alikusudia kuiwasilisha.
e. Tathmni mwendelezo wake.  Baini  kweli zile mwandishi alitaka  kuzielezea. Tambua jinsi alivyo kamilisha katika kuziwasilisha kweli hizo.
Jaribu kufuata mwongozo wake  na kuuendeleza katika mtindo huo.



f. Mkutadha wa kifungu..
 i.Maneno ya mbele nay a nyuma ya kifungu. Angalia jinsi mistari iliyotangulia na inayofuata inachosema. Chunguza aya kushusiana na sura nzima ambayo umetoka. Chunguza kifungu hicho katika nuru ya kitabu kizima ambamo kinapatikana.
Jifunze kiini na mazingira yote ya kitabu.
ii. Hali ya mila.  Je mila za wakati ule ziliathiri kile kilichoandikwa? Je watu walioandikiwa kifungu hicho awali wangekuwa na wazo la kile kilichoandikwa tofauti na ambalo tungepata katika hali yetu? Kama ndivyo nini ingekuwa maana inayolingana na sasa?
ii. Hali ya kihistoria. Je jambo hili liliandikwa lini?je wakati huo ulishawishi kile kilichoandikwa? Je matukio ya kwakati ule yaliyokuwa yakijulikana wakati ule wa uandishi yalikuwa na  maana maalum ju ya kile kilichosemwa?
iv.  Hali ya kijiografia.  Mwandishi alikuwa wapi wakati anaandika maneno hayo?je Watu walioandikiwa walikuwa wapi?Je mazingira yao yana uhusiano wa chochote katika kle kilichosemwa?
v. Biblia kwa ujumla.  Kila sehemu ya maandiko ifasiliwe kwa uaminifu na kwa umakini ili ikubaliane na maandiko yote. Andiko lolote lisifasiliwe nje ya mkutadha wake. Maandiko ni lazima yatafsiri maandiko.

E.Kupanga Maelezo.
Mpanglio mzuru wa maelezo na kazi  kwa ujumla ni wa faida sana kwa mhubiri. Hakikisha unapnga maelezo yako kimaantiki. Mpangilo mzuri wa kazi na mawazo humwezesha mhubiri kulielewa vizuri somo na kulishughulikia somo kikamilifu.
Pia huwawezesha wasikilizaji kulielwa somo na kulikumbuka somo .
1.      Ujumbe uwe katika mpangilio.Panga ujumbe wako katika mtiririko mzuri ili uweze kuufuata kwa urahisi wakati wa kuhubiri.
2.      Weka ujumbe wako katika hali ya kueleweka. Jitahidi kukamilisha vipengere vyote unavyohitaji kuviongelea katika mahubiri yako. Kabla ya kupanda mimbarini.
3.      Kazia katika mawazo. Unapaswa kuyaweka mawazo yakob katika sentensi fupi. Jifunze namna ya kuyaimarisha mawazo yako kwa pamoja nakuyaelezea katika sentensi fupi zinazoeleweka kwa urahisi.Jizoeze kupunguza na kulielezea wazo kwa sentensi moja.
4.      Tayarisha maelezo mafupi.Kumbuka kwamba maelezo yako yako ili kusaidia kumbukumbu yako.unapaswa kuwa na vidokezo vitakavyosaidia kulikumbuka somolako au ujumbe wako.
5.      Ufanye rahisi kuusoma. Ni vizuri kupiga chapa  mahubiri yako ili uweze kusoma kwa urahisi wakati wa ukihubiri. Pia waweza kutoa vipeperushi na vijarida kwa wasikilizaji wako ili waweze kufuatilia zaidi ujmbe au somo lako.


Zoezi.
1. Eleza maana ya mahubiri ya aya.
2.Tathmini ubora na udhaifu wa mahubiri ya aya.
3.Taja mambo mengine muhuimu ya kuzingatia katika mahubiri ya aya au kifungu licha ya yaliyotajwa katika kitabu hiki.
4. Andaa hotuba ya mahubiri ya aya na kisha hubiri kwa dakika kumi mbele ya wanafunzi wenzako.








II.    MAHUBIRI YA KUFAFANUA.
Mhubiri ya kufafanua ni aina ya mahubiri  ambaayo huhusisha kuchagua sehemu kubwa ya maandiko na kuicghunguza kwa undani na kuifasiri na kugungua kweli zilizomo katika sehemu hiyo ya maandiko na kushirikisha mkutano au usharika wako.
Mfano unaweza kuamua kupitia Injili yote  ya Luka  sura baada ya sura. Kuanzia sura ya kwanza, unatafuta kufasili na kuelezea maana na umuhimu wake mstari kwa mstari sura kwa sura mpaka umeimaliza yote.
Waweza kushughulikia sura moja kila wiki, na baada ya wiki kadhaa utakuwa umemaliza kitabu chote.Faida ya mahubiri ya ufafanuzi.

Hufanya mahubiri kuwa ya ki-Biblia.
1.      Yesu alitumia aina hii ya mahubiri. Alichukua kifungu cha Agano la kale na kufasili maana yake kwa wasikilizaji wake.
2.      Petro alitumia njia hii siku ya Pentekoste.
3.      Stefano alitumia njia hii.
Huwezesha waamini kuwa na msingi na uelewa mkubwa wa Biblia.Waamini huimalisha na huwa na ufshsmu mzuri na wa kina wa Neno la Mungu. Kwani kweli zote zilizomo katika kitabu kilichopitiwa tayari hufahamika vizuri kwa usharika wote.

Huvuta kuimalishwa na Roho mtakatifu. Roho mtakatifu hulithibitisha neno lake kwa ishara na miujiza sawasawa na Kweli zote zilizofunuliwa katika kitabu husika.

Humfanya mhubiri kuwa wa ki-Biblia. Mahubiri ya kufafanua humfanya mhubiri kuwa wa ki-Biblia kwani mhubiri huhubiri kile kilicho katika maandiko ya eneo husika. Mhubiri huwa anajikita katika mkutadha wa aya, sura na kitabu chote kwa ujumla. Hivyo kiini cha kitabu ndicho ambacho hubeba mahubiri yake yote.

Mambo ya kuzingatia katika kutayarisha mahubiri ya kufafanua.
I. Kwa umakini cuagua kifungu cha maandiko kinachostahili.  Hakikishwa kwamba kifungu hicho kitahudumia uzima na uwezo wa wasikilizajiwao.
1.      Usichague somo kwa sababu linakuvutia au kukupendeza.
2.      Usichage somo ambalo litazaa machafuko, mgawanyiko na mashindano.
3.      JItahidi kufanyika njia ili Mungu akupitie ili Mungu akupitie ili aweze kuongea Neno lake kwa watu wake kwa kupitia wewe.
4.      HIvyo basi unawajibika  kutafuta kujua mawazo ya Mungu kuhusu watu wake ambao amekupa wajibu juu yao.
5.      Huduma hii ni moja ya heshima kuu uliopewa lakini pia ni wajibu mkuu unaoogopesha sana. Hivyo basi unapaswa kuifanya kwa umakini wa hali ya juu.

II.Tafuta ujumbe unaolingana na hali ya watu ya wakati ule.
1.      Mungu kila mara huwa na ukweli wa sasa ambao hutaka kunena na watu wake.
2.      Mungu hukusudia jambo maalum kwa kila kundi la waamini
3.      Jifunze kujua kile Mungu anacho kwaaji ya kusanyiko kwa kilac wakati.



III. Jifunze sura ya kitabu kwa umakini.
1.      Soma sura unayo shughulikia mara nyingi mpaka umeielewa vizuri.
2.      Soma kwa uangalifu mstari hadi mstari.
3.      Kila kunapokuwepo na uhusiano wa wazi kati ya kifungu hicho na kifungu kingine unapaswa kusoma kifungu hicho ili uweze kupata maana zaidi. Maandiko hufasiri maandiko.
4.      Jenga usikivu kwa sauti ya Roho mtakatifu ili kupokea ufunuo toka kwake.

Tunia vitabu vya rejea ili kupatamsaada zaidi. Mfano. Itifaki ya Biblia, Kamusi ya Biblia, Biblia ya Tafsiri nyingine.Nk
IV. Kusanya taarifa  muhimu.
Waweza kupata vitu vingine muhimu vya kuhusisha kwenye somo lako kwa kutumia mbinu ya maswali  na majibu kama ifuatavyo.

1.      Nimewahi kusikia au kusoma nini juu ya somo hili?
2.      Roho mtakatifu amewahi kunionesha nini juu ya somo hili?
3.      Nimewahi kuona nini chenye uhusiano na somo hili ?
4.      Nimewahi kuwa na mawazo gani juu ya somo hili ?
Naweza kupata habari zaidi ju ya somo hili kwa nani au  wapi ? kueleweka.
5.       

V. Tambua kiini cha somo lako.
1.      Daima tafuta kugundua kiini cha sura unayoshughulikia.
2.      Tafuta kujua kile Roho mtakatifu alikusudia kuwasilisha alipoivuvia sura hiyo.
3.      Gundua undani wa somo hilo.
4.      Baini kile Mungu anataka kusema na watu wake kupitia sura hiyo.

VI.Kuwa na Lengo kamili.
Lengo lako daima lapaswa kuendana kikamilifu  na lengo la Mungu.
1.      Hakikisha kwamba Umegundua kile Mungu anataka kutoa kupitia maadiko hayo na kisha jizamishe katika kile Mungu anataka kufanya.
2.      Unapaswa kuhisi kile Mungu anachohisi Mungu humshirikisha mhubiri moyo wake na akili yake ili waweze kufanya kazi pamoja. Unapaswa kuchangamka.
3.      Fanyika chombo cha Mungu cha kupitishia ujumbe wake kwenda kwa watu wake.
4.      Kumbuka hukuitwa kushiriki mawazo yako na watu bali kuwashirikisha watu mawazo ya Mungu.

VII. Zungumza kulingana na ujuzi wako mwenyewe.
1.      Usitoe nadharia toa uhai. Hubiri kile ulicho na uzoefu nacho.kile ambacho umekifanyia kazi . wapaswa kuwa mtu kwa kwanza kula matunda ya kazi yako.
2.      Umeitwa kuwa barua Sio tu kwamba unataikwa kuuhubiri ukweli bali pia unatakiwa kuufanyia mazoezi na kuuonesha kwa matendo.
3.      Unapaswa kuwa mfano hai wa yote unayoyahubiri.

VIII. Upe maana ujumbe wako.
1.      Unawajibika kwa uwezo wako wote, kuhakikisha kwamba  maana ya kweli na umuhimu wa maandiko unakuwa wazi. Na wakueleweka kwa wasikilizaji.
2.      Daima jitahidi kuufanya ujumbe wako kuwa rahisi.
3.      Hivi ndivyo Yesu alivyofanya  Hii ilisababisha huduma yake kuwa na nguvu na mafanikio.
4.      Alichukua mambo yaliyokuwa mafumbo na  na akayaweka rahisi sana.
5.      Wahubiri wengine huyachukua masomo rahisi sana na  kuyafanya mafumbo magumu sana kiasi cha kutoeleweka kwa wasikilizaji wake au kuelewa kidogo.

IX.Fanya ujumbe wenye kutekelezeka.
1.      Daima unapohubiri jitahidi kuonesha wazi  wasikilizaji wako jinsi wanavyoweza kuutendea kazi ujumbe wako.
2.      Jitahidi kutoa ushauri wa kimatendo kuhusu watu wanavyotakiwa kumwitikia Mungu kwa namna ya kufaa.
3.      Husianisha mahubiri yako na maazimio yako kimatendo ambayo yaweza kuwafanya watu kuwa watendaji wa Neno na si wasikilizaji tu.


Zoezi

1.Eleza maana ya mahubiri ya kufafanua.
2. Tathmini ubora na udhaifu wa mahubiri ya kufafanua.
3. Taja mambo mengine muhimu ya kuzingatia katika mahubiri ya kufafanua.
4. Chagua sura mojawapo ya injili ya Yohana na kisha andaa mahubiri ya kufafanua kutokana na sura hiyo na kisha hubiri kwa dakika kumi.




III.    MAHUBIRI JUU YA MAISHA YA WATU.
A.Utangulizi
 Hii huhusu hadithi ya maisha ya watu. Kwa hiyo njia hii huhusisha mafunzo juu ya maisha ya watu mbalimbali tunaosoma habari zao katika Biblia. Kila hadithi ya mtu iliyoandikwa katika Biblia ina umuhimu kwetu. Maisha ya kila mhusika aliye kwenye Biblia yana  mafunzo kadhaa ambayo twaweza kujifunza.  Kila habari iliyoandikwa kwenye Biblia ipo kutufundisha kitu fulani ambacho ni cha thamani sana. 1Kor 10:1-11.
Mhubiri huchagua mhusika mmojawapo wa wahusika walio katika Biblia na kujifunza kwa kina kila kitu kilichotoke katika masiha ya mhusika huyo, tangu kuzaliwa kwake mpaka kufa kwake. Pia mhubiri hutakiwa kujifunza kuhusu nasaba na mbari ya mhusika huyo ili aweze kufahamu vizuri vitu vilivyomjenga na kumkuza mhusika, kisha hutayarisha mahubiri juu ya mhusika huyo na kuhubrikatika kusanyiko lake.
Mafundisho ya wahusika wa Biblia ni ya kushangaza na ya kuvutia.
Katkia aina hii ya mahubiri, mhubiri hupaswa kuchaqgua mhusika mmoja na kusoma habari zake zote zilizo kwenye Biblia na kisha huandikia kila wazo analolipata. Hapa mhubiri anapaswa kusoma kumbukumbuzote za mhusika katika Biblia.
Baada ya kusoma kumbukumbumbu hizo unapaswa kuanza kuweka pamoja mawazo yote unayoyapata katika utaratibu wa miaka yaani jinsi matukio yalivyotokea ya mhusika huyo.
B.  Faida za mahubiri juu ya maisha ya watu.
I.Hufunua ukweli wa maisha. Biblia imeelze wazi maisha ya wahusika  kama yalivyokuwa pale kuficha chochote. Imeeleza mafanikio yao na madhaifu yao. Ukweli wa maisha ya wahusika umewekwa wazi  na kwa uhalisia.
Wengi wa mashujaa wa biblia wanahitilafu zao za kibinadamu.Twajua kuwa walikuwa wanadamu kama sisi na walikutana na majaribu kama sisi.
Katika visa vyote vya historia kuna mtu mmoja mkamirifu ambae ni Yesu kristo pekee. Hata mashujaa wakubwa wa imani walikuwa na hitilafu zao. Hii inatupa kujua kwamba wao si tofauti na sisi.

Ni mifano ya kujifunzia.  Ni mifano na msada kwetu. Tunaweza kujifunza kutokananayo kuliko ujuzi wetu wa uchungu.

C.  Mambo ya kuzingatia
a)      Jifunze kuzaliwa kwa huyo mtu.
b)      Tafakali hali na mazingira aliyolelewa.
c)      Angalia uhusiano wake na Mungu katika maisha yake.
d)     Angalia jinsi alivyo wajibika kuhusu uhusiano wake na Mungu.
e)      Baini vitu alivyojifunza kutokana na mahusiano yake na Mungu.
f)       Tathimini mafanikio yake. Jifunze vitu vilivyomfanya afanikiwe.
g)      Tazama maeneo aliyokosea kama yapo. Na jifunze vitu vilivyomfanya akosee.
h)      Toa hitimisho kile tunachoweza kujifunza kutokana  na maisha ya mtu huyo.
Mambo hayo yote yanavutia na ni yenye vitu vingi vya Kutufundisha ambayo twaweza kujifunza  kutokana na watu hao. Tunaosoma habari za maisha yao katika Biblia.

D. Hatua za kufuata katika kuandaa mahubiri juu ya maisha ya watu.
I. Chagua mtu au msusika toka kwenye Biblia. Unapaswa kuanza na watu mashuhuli katika biblia ambao habari zao ziko wazi kabisa.kama vile Ibrahimu,Musa,Samweli,  Daudi, Yusufu, Debora, Miriamu, Mariamu, Dorkasi, Paulo, Petro. N.k.
Hawa ni baadhi ya watu ambao matendo yao yameyanyika kuwa nuru katika historia ya dushusiano kati ya Mungu na mwanadamu.
Kuna mambo mengi sana ambayo twaweza kujifunza kutokana na maisha yao. Aina hii ya mahubiri ni nzuri sana, kujifunza toka kwa wacha Mungu wenzetu waliotutangulia katiki wito na huduma hii ni jambo la msingi sana. 1Kor 10.1-11.
II. Chunguza maisha yake.
Anza kwa kusoma hadithi inayoelezea kuzaliwa kwa mtu huyo. Tafuta maana ya jina lake. Kwani jina lina maana sana ki-Biblia. Angslia kwa umakini kusudi la Mungu katka maisha yake. Ili uweze kuvumbua vitu vingi unapaswa kujiulza  mawsali fafuatayo:
1.      Mungu alitaka kutekeleza nini kupitia mtu huyu ?
2.      Je Mungu alifanya nini ili kusudi lake lijulikane kwa mtu huyu?
3.      Mtu huyu aliitikia vipi Mungu alipomjulisha kusudi lake?
4.      Tunaweza kujifunza nini kutokana na Mungu kuhusika katika maisha yake ?
5.      Kuna tahadhari zozote ambazo tunapaswa kuzichukua ?
6.      Je siri ya mafanikio yake ilikuwa nini ?
7.      Je mwisho wa maisha yake ulikuwaje ?
III. Chambua somo na kisha hubiri.
Baada ya kujiuliza maswali hayo  na kupata majibu utakuwa umepata vitu vingi ambavyo waweza kuvichambua kwa umakini na kuandaa somo kisha na kulihubiri somo hilo katika mpanglio na mtiririko Mzuri wwa mawazo.
Mwombe Roho mtakatifu akupe ufunuo zaidi unapokuwaukihubiri somo lako na lifanye somo lako kuwa na uhalisia katika maisha ya sasa ya wasikilizaji.

Zoezi
1.Eleza maana ya mahubiri ya wahusika au maisha ya watu.
2. Tengeneza orodha ya watu  mashuhuri walio katika Biblia. Orodha hiyo ihusishe wanawake na wanaume.
3. Tathmini ubora na udhaifu wa mahubiri ya wahusika.
4. Chagua mhusika mmoja wa kike au wa kiume na kisha andaa mahubiri kwa kumtumia mhusika huyo na kisha hubiri kwa dakika kumi.

IV.  MAHUBIRI YA MIFANO HALISI NA VIVULI.
Huu ni ujuzi unaohusu kuweka wazi au  kuchimbua  na kuwasilisha kweli uliojificha wa mifano mbalimbali katika Biblia.
Mfano ni kitu, mtu au tukio ambalo kinabii ni ishara ya kitu au mtu fulani.atakaetokea baadae. Inafanana au ni mfano wa Yule mtu au tukio.
Katika matumizi ya biblia ina maana ya mtu wa bibliaau tukio litakaloonesha kitu fulani kitakachotokea.
Mfsno mwanakondoo katika kitabu cha Kutoka ni mfano wa  Bwana Yesu.Kila kitu kuhusu kondoo wa pasaka kiunabii kilkuwa na maana ya ukombozi ya wajibu ambao Bwana yesu Kristo angetimiza.Yn 1:29.
Mifano ya biblia mara nyingi inaonekana kama kivuli(type) cha mambo yanayokuja baadae.
Ebr 8:5,10:1.
Siku takatifu pia katika agano la kale zilikuwa vivuli ju ya mambo ambayo yalikuwa yanakuja.
Kol 2:17. Hizo siku takatifu hazikukamilika zenyewe sehemu ya kusudi la kutimizwa kwake  ilikuwa ni kutanguliza sura ya kinabii ya vitu ambavyo vilikuwa bado vinakuja.
Kanuni za kutumia.
a. Unapojaribu kwa mara ya kwanza  kufundisha kwa kutumia mifano ya kwenye Biblia, zingatia misingi ifuatayo.
I. Tumia mifano rahisi zaidi. Anza na mifano rahisi mabayo maana yake iko wazi.
II.Endelea na tafsiri ya wazi.    Usijaribu kutafsiri kila kitu.Elezea ukweli wote kama ulivyo na wala si kutafuta kila kipengele chake na kukielezea kwa undani.
III. Usitumie maneno makavu. Usitumie mifano ya kufundishia kama kanuni.
IV.Sisitiza ukweli wa msingi..Usitumie nafai uliyonayo kwa kutoa mifano ya kufundishia. Mifano itumike kusisitiza mafundisho na si kutumia kama chanzo cha ukweli.
V. Uwe tayari kusahihishwa. Uwe tayari kusahihishwa na kukosolewa na wale waliokomaa kuliko wewe ili uweze kujifunza zaidi.
4. Kuelezea kusudi.
Ni njia ambayo kwayo mhubiri hupanua  maana ya ukweli ulio katika kifungu  maalum cha maandiko. Unatafuta naman ya kuuweka wazi ukweli ambao umejificha ndani ya kifungu. Hii njia nzuri sana ya kufundishia kusudi lote la ki-Mungu. Mdo 20:27.
Hapa mhubiri aweza kuchukua kitabu cha Biblia na kuelezea  maana yake sura baada ya sura.
Zoezi
1. Eleza maana ya vivuli na mifano.(Types).
2. Taja hatua za kufuata katika kutayarisha na kuhubiri mahubiri ya mifano na vivuli.s
3. Tathtmini ubora na udhaifu wa mahubiri ya mifano na vivuli.
4. Tayarisha mahubiri ya mifano na vivli na kisha hubiri kwa dakika kumi mbele ya wanafunzi wenzako.









V.   MAHUBIRI YA MADA.
Aina hii ya mahubiri hukusudiakutoa kiini  maalum kwa hadhira.Mhubiri huchagua somo fulani kisha huchunguza kila kitu ambacho Biblia inasema juu ya somo hilo. Baada ya kuchunguza na kuchambua kweli hizo huandikwa katika mapngilo wa somo.Mhubiri hupitia vifungu mbalimbali vya maandiko vinavyohusu somo hilo.
Aina hii ya amhubiri huhitaji maandalizi ya muda mrefu na utulivu mwingi. Pia huwasilishwa katika mfululizo wa vipindi kadhaa na si kimoja, kwa sababu ni vigumu kupitia kweli zote zilizo katika somo kwa kipindi kimoja tu.
Mfano wa mada za kuhubiri.
1.      Upendo wa ki-Mungu
2.      Ubatizo wa Roho mtakatifu
3.      Maombi ya kufunga.
4.      Nguvu ya usaidizi.
5.      Vita vya kiroho.
6.      Kutambua Ulimwengu wa roho.
7.      Kutembea katika mamlaka.
8.      Nguvu ya madhabahu.
9.      Kushughulikia majira na nyakati.
10.  Kutii mamlaka.

Mambo ya kuzingatia katika mahubiri ya mada.
1.      Uwe na ufahamu kwa kutosha juu ya somo husika.
2.      Fanya maandalizi ya mudamrefu nay a kina
3.      Unapaswa kuwa na lengo mahususi la mahubiri yako.
4.       Gawa somo  katika vipengele vidogovidogo.
5.      Kila kipengele laima kiwe na maandiko yanayokithibitisha na kukielezea
6.      Andiko liendane na  dondoo unayoitoa.

                                    


Zoezi.
Somo hili  lipo kimatendo zaidi. Kila mwanafunzi ashiriki katika kufanya mazoezi ya kuandaa mahubiri na ahubiri katika dakika zilizopendekezwa au mwalimu atakazopanga kulingana na muda uliop.
 Mwalimu anatakiwa kusimamia na kusahihisha kazi za wanafunzi na kutoa marekebisho katika maeneo ambayo wanafunzi hawajafanya vizuri.
1.Andaa Ujumbe kwa kutumia aina ya mahubi ya  mada na kisha hubiri mkuano kwa dakikika arabaini. Chagua mada yoyote.
2.Taja ubora na udhaifu wa mahubiri ya mada.
3. Taja mambo mengine matano  muhumu ya kuzingati katika kuandaa mahubiri ya mada.
4. Toa tofauti iliyopo kati ya mahubiri ya mada na mahubiri ya kufafanua.s












VI.MAHUBIRI YA MATUKIO.
Mahubiri ya matukio ni kipengele katika mahubiri ya maada, lakini kutokana na umhuhimu wake tumekitenga na kukielezea peke yake.
Mahubiri haya  ni mahubiri ambayo huandaliwa kutokana na tukio lilipoau ambalo litafanyika katika kipndi fulani.
Kiini cha mahubiri haya huwa ni tukio ambalo linafanyika katika ibada hiyo.Mfano wa matukio hayo ni
Tukio la,
1.      Kusimikwa kwa uongozi wa kanisa.
2.      Ndoa au kumuaga bibi arusi.
3.      Kubariki watoto.
4.      Ushirika mtakatifu
5.      Kuweka wakfu vitu mbalimbali.
6.      Kuhitimu mafunzo.(graduation)
7.      Msiba na mazishi.
8.      Sikukuu mfano Pasaka, mwaka mpya, N.k
Mambo ya kuzingatia
1.      Mahubiri haya yanapaswa kuendana na tukio husika.
2.      Mhubiri anatakiwa kufahamu ratiba nzima ya tukio hilo au shughuli hiyo.
3.      Mhubiri ahubiri kulingana na tukio husika.
4.      Mhubiri aepuke kutumia muda mwingi katika mahubiri.
5.      Mhubiri ahubiri kwa lugha itakayoeleweka na kusanyiko lote na lugha yapaswa kuwa rahisi.
6.      Mahubiri yapaswa kugusa kusanyiko lote.
7.      Mhubiri anapaswa kubiri kwa upendo.
8.      Mhubiri azingatie ratiba  ya tukio.

ZOEZI.
1. Chagua tukio mojawapo na kisha andaa mahubiri juu ya tukio hilo na hubiri kwa dakika 10
.2. Taja mabo mengine kumi ya kuzingatia katika mahubiri ya matukio.
3.Eleza ubora  na udhaifu wa mahubiri ya matukio.





















1. MAHITAJI YA MUHUBIRI:
a. Anapaswa kuwa ameokoka yaani amezaliwa mara ya pili.
a. anapaswa kuwa na wito  kamili na uliowazi kwajijli ya kazi hii na sii taaluma tu.
Anapaswa kuwa amejazwa Roho mtakatifu.
Anapaswakuwa na wito uliowazi kwake na kwa watu wengine pia.

3. Mhubiri anapaswa kuboresha utu na wito wake  kwa njia zifuatazo:
I.kuwa na ushirika  wa karibu na Mungu daima.
a)      Maombi na kutafakari Zab 1, Yosh 1:8.
b)      Kuishi maisha matakatifu.
c)      Kuwa mnyenyekevu daima.


II Anatakiwa kujifunza daima.
 Neno la Mungu na vitabu vinginevyo vizuri.
a)      Panga muda wa kusoma (soma kwa bidii).
b)      Pata chakula kwajili yak o mwenyewe.
c)      Pata chakula kwaajili ya watu wengine.
d)     Hudhuria makongamano na semina mbalimbali.
e)      Jifunze toka kwa wahubiri wengine wakubwa na wazuri waliokutangulia.


III.Jifunze kutokana na watu wanaokuzunguka na mazingira yao.
a)      Tazama na soma watu wanavyoishi, matatizo wanayokutana nayo.
b)      Fungua macho yako kujifunza kila mahali.

      IV.. Endeleza vipawa vyako vya asili.
Kil;a mtu anacho kipaji cha asili. Ni muhimu kuendeleza kipaji ulichonacho kwaajili ya utukufu wa Mungu. Mfano wa viapji vya asili ni Kuimba, kupiga muziki, kushauri, n.k. Vipaji vyote vyaweza kuendelezwa kwa njia ya mafuzo na mazoezi. Hivyo hakikisha unakuza na kuendeleza kipaji chako cha asili.

V..Tunza afya yako. Ni muhimu kwa muhubiri kutunza afya yake kwanibila kuwa na afya bora muhubiri hataweza kutimiza wito wake kwa ufanisi.  Pai ni jambo jema kwa muhubiri kufuata ushauri wa kitaalamu yaani kuchunguza afya yake mara kwa mara ili kushugulikia mapema kama kuna dosari zozote za kiafya kiwa bado change. Pia ili muhubiri aweze kuwa na afya bora anatakiwa kufanya yafuatayo:
i. kula chakula bora.
ii. Kufanya mazoezi mra kwa mara.  Mfano kukimbia, kuruka, kutembea, N.k
iii. Kuwa na muda wa kupumzika.( Muhubiri ni lazima awe na muda  wa kutulia na familia yake. Pia mhubiri anapaswa kuwa na likizo.)


VI. Vipaumbele vya muhubiri. Unapaswa kutambua vipaumbele na uviheshimu ili uweze kuwa na ufanisi katika huduma na wito wako. Vpaumbele hivyo ni:
a)      Mungu.
b)      familia.
c)      Huduma
d)     Watu wengine.
Kila kipaumbele kipe nafasi yake. Usipofanya hivyo utumishi wako utatyumba.

VII. Ni lazima amtegemee kikamilifu Roho mtakatifu.
 “ Atatwa katika yaliyo yangu na kuwapa ninyi. Yn 14:26,  16:13-14.

  Hivyo ni lazima mhubiri ajifunze kumtegemea Mungu  kiamilifu;
a)      Katika maisha yake ya kila siku.
b)      Katika masomo yake.
c)      . Katika maandalizi na matayarisho.
-          Katika kuandaa hotuba za kuhubiri.
-          Katika kuandaa matirio ya kutumia katika kuandaa hotuba zake.
-          Katika kuwasilisha hotuba zake.
a)      Kwa kutumia stadi na ujuzi pekee wa homiletics na akili yako pekee kusanyiko lako litabaki tupu na ukiwa.
b)      Ni Roho mtakatifu pekee anaewweza kumtia nguvu mhubiri kuufikia ushindi wa kiroho Mdo 1:8.
c)      Ni Roho mtakatifu pekee anaeweza kubadilisha na kuhuisha wasikilizaji wako. Yn 16:7-8.

d)     Mhibiri unapaswa daima kumtegemea kikamilifu Roho mtakatifu katika kazi na wito wako wa uhubiri. Hakikisha unashirikiana nae kikamilifu iliuweze kuwa na ufanisi katika wito na huiduma yako.

*Roho mtakatifu aweza kuwa msaada kwa mhubiri  lakini yeye ni kama hua….






MADA YA PILI.
A. mhubiri ni mtangaza ujumbe wa Mungu.
-Yeye ni msemaji wa Mungu. Husimama katika nafasi ya mungu na kuzungumza kwa niaba yake Mungu.
B. Biblia ndiyo asili ya ujumbe. Ujumbe wowote uaouhubiri nilazima utokane na Biblia nje ya Biblia si mahubiri bali ni masimulizi tu.
-Ikiwa kuhubiri ni kutangaza  ujumbe wa  Mungu mhubiri anapaswa kwenda mahali Mungu alipoongea mara nyingi  na waziwazi  yaani “Biblia” 
Kwa njia nyingine kuhubiri ni kuipa Biblia sauti.ni kuacha Mungu aongee mwenye koa kwa Neno lake.
Kwa nini Biblia peke yake?  Kwanini si kitu kingine toka vitabu vizuri vya kikristoau toka magazeti au maelezo na masimulizi ya mtu maarufu na aliye mkuu.
1. Biblia ni maoni ya Mungu kwa kila jambololotelililotolewa.
(Mhubiri aliye kuwa amekosolewa kwaajili ya hotuba yake alisema “hata mimi sikuipenda pia lakini  haikuwa maneno yangu na nilikuwa sitoi mawazo yangu bali kile Mungu amesema katika Neno lake. Kwahiyo nilitoa mawazo ya Mungu na si yangu.).
Kuhubiri hotuba ya ki-Biblia humpa mhubiri ujasiri mkubwa. Kutangaza kwa nguvu;
·         Biblia inasema ………………….
·         Mungu anasema…………………

2. Neno la Mungu lina nguvu. Wab 4:12.
3.Neno la Mungu ni kama mbegu.sBiblia hukutana na kila hitajila mwanadamuna matatizo yake yote yanayomkabili.
5. Inampendeza Mungu- Neno lake lililovuviwa  amri yake ilikuwa wazi
“Enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi na muwafundishe kuyashika yote niliyowaamuru”
6. Roho mtakatifu hulithibitisha Neno la Mungu.
C. jinsi ya kupata maandiko ya Kuhubiri.
Mwombe Mungu Akupe ujumbe waq kuhubiri.kissha pokea andiko toka kwa Mungu kuhusu mahubiri hayo kwanini yeye Mungu anajua mahitaji ya watuya sasa yanayotakiwa kushughulikiwa……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
D. Namna ya kutumia maandiko kwa usahihi.
Kufasili na kutumia maandiko matakatifu  kwa maana yake halisi ni kazi moja muhimu na takatifuambayo mhubiri anawajibu wa kuifanya.
1. Usipindishe wala kugeuza maana ya andiko ili kulifanya andiko likubaliane na mawazo yako.
2.Usichukue sehemu ya andiko na kuifanya iseme kitu ambacho hakiendani na mkutadha wake ambao ambacho mkuadha hauoneshi kuwa ni maana yake halisi.
3. Soma andiko kwa umakni (zingatia sarufi na misemo iliyomo katika andiko) na ulitafakari katika maana yake halisi.
- Baini aina ya tungo zilizotumika na aina za maneno yaliyotumika kuunda tungo hiyo.
-Tazama maneno maalumu(Key word)yanayotokeza katika andiko unalotafakari.Mfano DAmu, Msalaba, Yerusalemu N.k.
-Kuwa makini kutazama tamathali za semi zilizotumika au kujitokeza. Mfano. Misemo, nahau, tashibiha, tashihisi tashititi, tafsida ,methali n.k.
4. Soma andiko katika mkutadha wake wa sasa.  hapa unatazama mkutadha wa msitari, aya na sura ya andiko.
5.Soma andiko katika mkutadha wake wote. Hapa unatazama mkutaqdha wa kitabu. Waweza kutumia mAswali kadha katika kutazama mkutadha wake mfano  Ninin dhamira ya kitabu au waraka huu wote? Tazama historia, jografia na utamaduni wa wakati wa Biblia hii daima yaweza kuwa msaada.
* Daima kumbuka kuwa mafundisho ya Biblia yanapatana na hayapingani kamwe. Hayajipingi yenyewe kwa yenyewe lakini ufuno wake ni endelevu.
*Mafundisho ya agano la kale ni lazima yafasiliwe katika nuru ya Agano jipya. Kushindwa kufanya hivyo kumesababisha kuzaliwa kwa mafundisho mengi ya uongo.(Religious cults).
Mfano. Kutunza sabato, kutokula baadhi ya wanyama, Kuabudu sanamu, kuoa mitala N.k
D. mawazo mawili potofu kuhusu mahubiri.
Kuna dhana mbili potofu ambazo zinajitokeza katika uwanja na taaluma ya mahubiri mawazo hayo ni:
a. Maaandalizi si lazima. Wazo la kwanzalenye makosa  ni kwamba maandalizi si lazima na huonesha kukosa imani kwa mhubiri. Watu wenye kushikilia msimamo huu hufikili kwamba imani ya kweli  hutupilia mbali  jitihada yoyote inayojaribu kuandaa akili na hiyvo husimama mimbarini  wakiamini kwamba Mungu atawapa maneno ya kusema.husimamia maawazo haya:
i. Roho mtakatifu atakupa unachohitaji kuhubiri. Unapopanda mimbarini.
_- Zab 81:10 “  Fumbua sana kinywa chako name nitakijaza”(Hutumia andiko hili kutetea msimamo wao.).
Pia husema kwamba Yesu alisema kwamba “Msifikirifikiri nini cha kusema maana mtapewa kinywa cha usemi saa ili ilie mnapotakiwa kusema”
 Unapoyachunguza kwa umakini maandiko hayo utagundua kwamba  maandiko hayo wanayafasili nje na mkutadha wake na na kulazimioshwa yaseme kile ambacho hayamaanishi.
*Mahubiri ni kamana jengola kiroho ambalo linatakiwa kusanifiwa na kuandaliwa chini ya uongozi wa  Roho Mtakatifu. Roho mtakatifu ndiye mhandisi mkuu wa mahubiri.
b. Uwezo wa mtu unatosha. Kuweka mkazo katika matayarisho  na kutegemea uwezo wa   kibidanu tu. Wahubri wanaoshikilia msimamo huu hudai kwamba  maandalizi peke yake yanatosha  na huweka mkazo kwenye  matayarisho pekee.Kumtegemea Roho mtakatifu huwa ni kudogo sana au hakuna kabisa, bali tumaini la mtu binafsi ambalo ni matokeo ya kujifunza na kuendeleza uwezo wa asili.
Ujumbe wa namna hii waweza kuwa mzuri kabisa lakini hauwezi kuleta matokeo yatakikanayo daima. Kwani ni Roho mtakatifu pekee ndiye anaeweza kuleta badiliko katika maisha ya waikilizaji wako. Bila yeye mahubiri huwa ni maiti na haiwezi kuleta uhai kwa sababu ni uhai wenye uwezo wa kuzaa uhai.
*Roho mtakatifu huuhuishaujumbe na kuletaq matokeo yaliyokusudiwa na Mbingu katika maisha ya wasikilizaji.
Ili mhubiri aweze kuhubiri sawasawa anapaswa kuwa na maansdalizi ya kutosha katika kuuandaa ujumbe wake kwa kusoma, kutafakari na kuchambua kweli zote zilizomo katika ujumbe wake. Lakini hayo yotec anapaswa kuyafanya akiwa katika hali ya maombi.
Mhubiri anapaswa kumsikiliza Roho mtakatifu klwa kina na kupata uongozi kwake na kutaka Roho mtakatifu amshirikishe kile anachotaka kusema na watu wake na kukifanyia uchambuziyakinifu katika hali ya maombi ili aweze kukiwasilisha kwa ufanisi.
·         Mhubiri anapaswa kutambua kwamba yeye hana watu wala si Chanzo cha ujumbe. Kwasababu hiyo anatakiwa kumsikiliza mwenye watu  na aliye chanzo cha huo ujumbe na kusimama katikati kwa uaminifu kuwafikishia watu kwa usahihi kile mwenye watu anachotaka kiwafikie watu wake.
·         Mhuibiri anapaswa  kutambua kwamba kazi ya kuhubiri ni takatifusana na ni kazi nyeti ambayo yapaswa kufanywa kwa umakini, uaminifu na unyeyekevu mkuu.
·         Mhubiri mwenye kutegemea juhudi zake na uwezo wake wa asili atakuwa ni muhubiri kilema na halikadharika mhibiri mweye kutegemea kupewa ujumbe akiwa mimbarini atakuwa ni kilema.
·         Vyote viwili vyapaswa kwenda pamoja, maombi na matayarisho.Kwa sababu mahubiri ni matokeo ya mawasiliano na ushirika mzuri kati ya  Roho mtakatifu na mhubiri.

Aina za mahubiri.
 Katika kipenele hiki tutaeleza aina saba za mahubiri. Ni vizuri kwa mhubiri kufahamu aina zote za mahubiri. Hii itamsaidia kuwa  na uhuru waq kutumia ainayoyote katika huduma yake na kufanya huduma yake kuwa ya kuvutia kwa watu wanaomsikiliza.

2. Mahubiri ya mada.
Aina hii ya mahubiri hukusudiakutoa kiini  maalum kwa hadhira.Mhubiri huchagua somo fulani kisha huchunguza kila kitu ambacho Biblia inasema juu ya somo hilo. Baada ya kuchunguza na kuchambua kweli hizo huandikwa katika mapngilo wa somo.Mhubiri hupitia vifungu mbalimbali vya maandiko vinavyohusu somo hilo.
Aina hii ya amhubiri huhitaji maandalizi ya muda mrefu na utulivu mwingi. Pia huwasilishwa katika mfululizo wa vipindi kadhaa na si kimoja, kwa sababu ni vigumu kupitia kweli zote zilizo katika somo kwa kipindi kimoja tu.




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

NOTICE FORM FOUR

MICROSOFT EXCEL